Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAKAMU
wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Malawi ambalo
litafanyika Julai 26 hadi Julai 27 mwaka huu mkoani Mbeya.
Kongamano
hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na
Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania(TanTrade) pamoja na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya
Malawi(MITC).
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za TIC, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Amos Makalla amesema kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Kuimarisha
Uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi" huku lengo
la kongamano hilo likiwa kuwatanisha wafanyabiashara /wawekezaji wa
nchi hizo mbili ili kubaini fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji.
Ambapo
amefafanua zitawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za
viwanda ,usafirishaji,utalii, uvuvi, kilimo ,madini, elimu, afya, benki,
mawasiliano, tehama na biashara kwa ujumla.
Pia
amesema sambamba na kongamano hilo kutakuwapo na mikutano ya
wafanyabiashara (B2B), mikutano ya watendaji wa Serikali(G2G) na
mikutano kati ya Serikali na wafanyabiashara (B2G) kutoka nchi hizo
mbili.
"Tayari
mkoa wa Mbeya umeona umuhimu wa wa kongamano hili na una kila sababu za
kuandaa na kuratibu kwasababu unaona fursa na mkoa upo tayari kwa kuna
miundombinu yote muhimu,'amesema Makalla.
Ameongeza
katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji Serikali kupitia
Mkoa wa Mbeya tayari imeanza kufungua milango ya uwekezaji kwa kuwekeza
katika miundombinu ya kiuchumi ikiwamo uwepo wa meli mbili ambapo moja
ya mizigo na nyingine ya abiria inatengenezwa katika bandari ya Itungi
na kuanza ujenzi wa kituo kimoja cha forodha katika mpaka wa Kasumulu.
Pia
Makalla amesema Serikali imekwishatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa
bandari kavu katika eneo la Inyala kwa lengo la kuwezesha upokeaji na
uhifadhi wa bidhaa moja kwa moja kutoka bandari ya Dar es Salaam.
Akifafanua
kuhusu komgamano hilo Makalla amesema ni bure kwa washiriki isipokuwa
wadau wenye nia ya kushiriki wanahamasishwa kupakua na kujaza fomu ya
usajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambayo ni www.mbeya.go.tz na baadae kuziwasilisha kwa barua pepe kupitia ;ras.mbeya.go.tz.
Pia kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania ambayo ni http://www.tic.go.tz.displayListPublication na baadae kutuma kwa diana.ladislaus@tic.go.tz/ au tovuti ya TanTrade ambayo www.tantrade.go.tz na kisha kutuma kwa info@tantrade.go.tz.
Pia kupitia tovuti ya Kituo cha Biashara na uwekezaji Malawi ambayo ni https://mitc.mw/ na kisha kutuma kupitia anuani ;info@mitc.mw.
"Fomu
hizo ziwasilishwe kwa barua pepe zilizoanishwa kabla ya Julai 16 mwaka
huu.Tunaomba wadau wote kushiriki ili kuibua fursa za uwekezaji na
kibiashara kwa faida za wananchi wote,"amesema Makalla.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati
ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya,
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) John Mnali.
Baadhi
ya watendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (hayupo pichani) kuhusu kongamano la
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai
26 na 27 jijini Mbeya.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Amos Makalla na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
No comments:
Post a Comment