CMSA yairudisha NICOL soko la hisa
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne , Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameishauriwa Mamlaka
ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kutoa elimu kwa watanzania
kuhusiana na ununuaji wa hisa katika soko la hisa.
Kikwete
ameyasema wakati hafla ya Kampuni ya NICOL kurudishwa katika Soko la
Hisa Dar es Salaam(DSE) baada ya kukidhi vigezo vya kisheria kuongia
katika soko hilo, amesema CMSA ikitoa elimu kwa wananchi kutafanya
kuongeza hamasa ya ununuaji hisa kuliko ilivyo sasa.
Dk.Kikwete
amesema kuwa CMSA ikitoa elimu kutafanya kampuni nyingi kuorodheshwa
katika soko la hisa na kufanya uwekezaji wa miradi mingine.Aidha
amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia katika masoko CMSA imeshauriwa
kuboresha zaidi manada wa soko la Hisa wakati wa kufungua na kufunga.Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alisema kwamba lengo la kuisajili Nocol ilikuwa ni kuwasaidia .
"Nakumbuka
wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa
kuhoji kwanini nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii
ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo,"
alisema.Kikwete kwamba hakuwahi kuusikia mgogoro wa NICOL wakati wa utawala wake.
"Lengo
lilikuwa kusaidia wazawa kujijenga kuichumi na kukuza maendeleo,
nimesikia leo (jana) hadithi ya Nicol katika uongozi wangu sikusikia
kabisa mgogoro wao," alisema Kikwete.Aidha aliipongeza CMSA kwa utendaji kazi wake, ikiwemo kusimamia kwa madhubuti masoko ya mitaji.
Nae
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana
(CMSA), Nicodemus Mkama,amesema kuwa imefanikiwa kuorodhesha hisa
69,165,170 za Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ya National Investment
Company Limited (NICOL) katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ni
kutokana na kukidhi vigezo vya kisheria .
Amesema
NICOL iliondolewa katika orodha ya kampuni ya kampuni zilizoorodheshwa
DSE Juni 2011 kutokana na matatizo ya kiutendaji katika uwekezaji katika
uwekezaji.mamlaka iliidhinisha mauzo ya awali ya hisa za Kampuni ya NICOL kwa umma yaani (Initial Public Offers – IPO).
Amesema
kwamba mauzo hayo yalifanyika katika awamu mbili, moja ikiwa ni Novemba
2004 ambapo Kampuni NICOL ilifanikiwa kukusanya sh. bilioni 3.9 na
awamu nyingine ilifanyika Oktoba mwaka 2007, ambapo jumla ya sh. bilioni
5.6 zilikusanywa.
"Kutokana
na mwenendo mzuri wa mauzo ya hisa, Kampuni hii ilifanikiwa
kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar Es Salaam Julai 15, 2008. Hata
hivyo, kutokana na matatizo ya uongozi na kiutendaji katika
uwekezaji,kampuni hii tuliiondoa sokoni Juni mwaka 2011 na CMSA iliamuru
kuwasimamishwa kwa Wakurugenzi wa Bodi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya NICOL ili kuwezesha uongozi mpya kuteuliwa na wanahisa
wote,"alisema.
Mkama
alisema kwamba Aprili 14, 2012, Kampuni ya NICOL ilifanikiwa kupata
uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk. Gideon Kaunda na ofisa
Mtendaji Adam Kinoni ambao ulithibitishwa kupitia Mkutano mkuu wa
wanahisa wote.
"Uongozi
huu umeweza kushughulikia matatizo ya uendeshaji wa kampuni na
uwekezaji ambayo yalisababisha Kampuni hii kuondolewa katika soko la
hisa,NICOL pia imeweza kutekeleza maelekezo yote yaliyokuwa yametolewa
na CMSA Mamlaka ili kukidhi hadhi ya kuendelea kuwa kwenye Soko la Hisa.
Mkama
aliyataja masharti ambayo CMSA ilitoa kwa NICOL nikutoa notisi kwa
wanahisa kuwaelezea kile kinachoendelea ndani ya kampuni na kutayarisha
mkutano mkuu wa wanahisa,kuhakikisha mahesabu ya NICOL tokea mwaka 2009
yanakamilishwa kama ilivyopangwa, Kuteua wakaguzi wa nje (External
Auditos) kwa ajili ya hesabu za kampuni kwa miaka ya fedha 2010-2015 ili
kuhakikisha kuwa mkutano mkuu unafanyika Octoba.
Amesema
masharti mengine waliyowapa ni Kutayarisha taarifa ya shughuli za
kampuni ikiwemo kuiwezesha kuanza kutekeleza kazi zake na kuangalia
uwezekano wa kuirudisha kampuni sokoni.
Mkama
alisema NICOL imefanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati
mpya wa uwekezaji unaohusisha kuugawa uwekezaji wake kwenye dhamana za
serikali kwa lengo la kupata anuwai, kuleta ulinzi wa mtaji na uongozi
madhubuti.
"Mageuzi
makubwa ya kiutendaji na matokeo mazuri ya mwenendo wa Kampuni ya NICOL
ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa CMSA uliodhihirika katika
kusimamia sheria, miongozo na kanuni za masoko ya mitaji. Misingi hiyo
ndiyo iliyotumika kuiwakilisha serikali kulinda masilahi ya wawekezaji
katika kampuni ya NICOL, na hivyo kukuza thamani ya uwekezaji kutoka sh.
4.6 bilioni Mwaka 2004 mpaka Sh. Bilioni 96.2 mwaka 2017, sawa na
ongezeko la asilimia 1,991,"alisema.
Mwenyekiti
wa DSE, Jonathan Njau, alisemakwamba DSE wana furaha kuiona Nikol
ikirejea tena katika soko la hisa kwaajili ya kuuza, kununua, na kukuza
uchumi wa kampuni pamoja na taifa.
Aliwaasa
viongozi wa Nicol kufuata taratibu ikiwa wanataka kuendelea kukaa
katika soko lazima wafuate sheria na utaratibu ikiwemo kutengeneza
mahesabu na kukaguliwa kwa uwazi.Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda, alisema kwamba wamerudi sokoni kwa kasi hivyo itauza, kununua na kuzalisha zaidi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akigonga kengele kwa ajili ya kufungua soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuingia kampuni ya NICOL.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika Soko la Hisa la Dar es Salaam , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika soko hisa na changamoto walizoweza kukabiliana nazo .
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
No comments:
Post a Comment