Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Mfumo
wa Usimamizi wa Fedha za Umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa toleo
la 10.2 (Epical 10.2 ) umetajwa kuchochea utekelezaji wa dhana ya
uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma .
Akisoma
hotuba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, Afisa
Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza amesema kuwa mafunzo ya mfumo
wa Epicor 10.2 yatasaidia kuongeza tija katika utendaji kutokana na
mfumo huo kuandaliwa mahsusi kuungana na mifumo mingine ili kukidhi
matakwa ya maboresho yanayofanywa katika usimamizi wa fedha za umma.
Mafunzo
hayo yanawashirikisha wahasibu, maafisa ugavi, na waweka hazina wa
mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukw, ns yanaendeshwa na Serikali ya Tanzania
kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa
Uimarishwaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3, unaosimamiwa na Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani ( USAID), .
Hivi
sasa, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini zitatumia mfumo mmoja wa
uhasibu ujulikanao kama mfumo wa usimamizi wa Fedha za Umma, toleo la
10.2 utakaosaidia kuhakikisha kuna mfanano katika uhasibu,utoaji wa
taarifa na usimamizi wa fedha.
“Mafunzo
haya yana lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia mapato na
matunizi ya fedha za umma kwenye Halmashuri na pia kuwapatia uelewa wa
mabadiliko ya msingi yaliyofanyika bila kukwamisha utoaji wa huduma kwa
wananchi” Alisisitiza Ntigeza
Akifafanua
Bi. Ntigeza amesema kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa watahakikisha kuwa
kuna matumizi sahihi ya mifumo kuanzia ngazi za vituo vya kutolea
huduma kuanzia mkoani hadi ngazi ya Halmashuri zote.
Aliongeza
kuwa awali maafisa katika maamlaka za Serikali za walilazimika kupitia
mipango na bajeti katika mfumo mmoja, mapato katika mfumio mwingine na
matumizi kwenye mfumo mwingine, hivyo kuleta ugumu katika
uwajibikaji,ufanisi, na thamani ya fedha katika matumizi ya fedha za
Serikali.
Mfumo
wa Epicor 10.2 utaunganishwa na mfumo unaowezesha malipo yote kufanyika
kwa njia ya kielektroniki, Mfumo pia unwezesha matumizi yote
yanayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika vituo vya Afya na
Shule kuhifadhiwa na kuwekwa wazi kwa vituo vya kutolea huduma pamoja na
jamii wanayoitumikia.
Kwa
upande wake Afisa Usimamizi Fedha kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.
Mmaka Mwinjaka amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza uwazi ,
uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa kwa wakati hivyo kuondoa
ubadhilifu.
Aliongeza
kuwa EPICA 10.2 ni mfumo ulioboreshwa ili kuweza kuongea na mifumo
mingine kama ile ya ukusanyaji mapato na ule wa kupanga bajeti, mipango
na kutoa ripoti yani PlanRep.
Kuanzia
Julai 2018, Serikali ya Tanzania itaanza kutumia mfumo mpya wa uhasibu
kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 za Tanzania bara, Mradi wa
Uimarishji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano
unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara. PS3
inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya
mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii
zenye uhitaji.
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akisisitiza umuhimu wa
Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2
kwa wahasibu, waweka hazina, Maafisa Ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe
na Rukwa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja
leo Jijini Mbeya wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mkuu
wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za
Umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusu mfumo wa Usimamizi
wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 utakavyosaidia kuboresha
utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa leo Jijini Mbeya wakati wa
hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Afisa Elimu Mkoa
wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla
ya ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor
toleo la 10.2 yanayofanyika Jijini Mbeya yakiwashirikisha Wahasibu,
Maafisa Ugavi na Waweka Hazina kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.
Afisa
Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akifungua mafunzo kuhusu
Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor toleo la 10.2 niaba ya
Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja leo Jijini Mbeya. Mafunzo
hayo yanawashirikisha wahasibu, waweka hazina, maafisa ugavi wa
Mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa .
Mkuu
wa Timu ya Mifumo kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za
Umma (PS3) Bw. Desderi Wengaa akiagana na Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya
Bi. Paulina Ntigeza ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu
Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja leo Jijini Mbeya katika hafla
ya ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa Epicor
toleo la 10.2 kwa wahasibu, waweka hazina, Maafisa Ugavi wa Mikoa
ya Mbeya, Songwe na Rukwa
Afisa
Elimu Mkoa wa Mbeya Bi. Paulina Ntigeza akiwa kwenye picha ya pamoja
na washiriki wa mafunzo kuhusu Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma wa
Epicor toleo la 10.2 yalishirikisha wahasibu, waweka hazina,
Maafisa Ugavi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe leo Jijini Mbeya.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya)
No comments:
Post a Comment