Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), imeamua kubuni na kuzindua mashine maalumu ya kutengenezea mkaa mbadala.
Lengo
la kubuni mashine hiyo ni jitihada za DIT katika kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mikakati yake ya kukabiliana na
uharibufu wa misitu na utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia
kuhusu umuhim wa mashine hiyo leo kwenye Maonyesho ya Wiki ya Mazingira
yanayoyendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mkufunzi
wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo wa taasisi hiyo Asaph Kagina, amefafanua
mashine hiyo yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani tatu za mkaa kwa
siku ni suluhisho tosha katika kulinda misitu hapa nchini.
Amesema
kuwa mashine hiyo inayotumia mabaki ya mazao mashambani, zikiwemo pumba
za mpunga, mahindi, vifuu vya nazi, pumba pamoja na makaa ya mawe,
imeundwa kutokana na wazo lilitokana na ripoti maalumu ya Banki ya Dunia
kuhusu hali ya mazingira, pamoja na ripoti nyingine ya aliyewahi kuwa
Mkurugenzi wa Misitu na nyuki Dk. Felician Kilahama.
Amefafanua
ripoti ya Dk.Kilahama imeeleza wazi kuwa iwapo kasi ya ukataji miti
itaendelea kwa kipndi cha miaka 10 Tanzania hakutakuwa na misitu ya miti
na hivyo DIT kupitia watalaamu wake wameona haja ya kutafuta njia
mbadala ya kupata mkaa ambayo itakuwa sahihi katika kulinda mazingira
"Ni
mashine ambayo tuaamini kama ikitumika ipasavyo itatoa mchango mkubwa
kwa Taifa katika kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ambalo
kwa kipindi kirefu limekuwa na athari kubwa huku likihatarisha hatari ya
kutokea jangwa katika miaka kadhaa ijayo" amesisitiza Kagina.
Amesema
mashine hiyo maalumu imetengenezwa na wanafunzi watatu wanaosoma katika
taasisi hiyo waliokaa chini na kuja na wazo la kutengeneza mashine hiyo
ili kutimiza ndoto zao za ulinzi wa mazingira na misitu kwa ujumla,
kitu ambacho wamefanikiwa.
Aidha
alisema mashine hiyo inayotumia nishati ya umeme pamoja na dizeli,
imeundwa kwa kuzingatia mazingira ya mijini na vijijini huku ikivilenga
zaidi vikundi mbalimbali vya ujasiramali ili kuviwezesha kuja na mradi
huo utakaovisaidia kujitengenezea faida.
Alisema
gharama za ununuzi wa mashine hiyo inatokana na uhitaji wa mteja kwa
kuzingatia ukubwa, huku gharama ya juu kabisa ikiwa ni cha Sh Milioni 5,
na ikiwa na uwezo wa kutengeneza faida kuanzia kiasi cha Sh 900,000 kwa
siku moja.
Ameziomba
taasisi za kifedha kuwasadia wajasiriamali kwa kuwapa mikopo ili waweze
kununua mashine hiyo na hivyo kujikwamua kiuchumi sambamba na kuunga
mkono juhudi za kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.
Michuzi
Blog imeshuhudia idadi kubwa ya wananchi ambao wanafika kwenye viwanja
hivyo kufika banda la DIT ambapo pamoja na kuelezwa mambo mbalimbali
yanayofanywa na taasisi hiyo wengi wao wamekuwa na shauku ya kutaka
kujua zaidi kuhusu mashine hiyo ambapo baadhi yao wameelezea matumaini
yao kuwa ikitumika vizuri itakuwa mkombozi katika kulinda mazingira
nchini.
Mkufunzi
wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam(DIT)akifafanua jambo kwa baadhi waandishi waliotaka kufahamu kwa
kina machine ya kuzalisha mkaa mbadala ambayo imebuniwa na taasisi hiyo
Mkufunzi
wa Idara ya Uhandisi Mitambo Katika Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam(DIT) Akita maelezo ya machine maalum ambayo imebuniwa na taasisi
hiyo ambayo inazalisha mkaa mbadala
Mashine ya kutengeneza mkaa mbadala ambayo imebuniwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
No comments:
Post a Comment