Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mabasi Tanzania(TABOA) Enea Mrutu
amewaomba wamiliki wote wa mabasi nchini kuendelea kutoa huduma za
kusafirisha abiria kwa umakini wa hali ya juu kwa kuhakikisha
hawasababishi ajali wakati wakiendelea kusubiri kukuona na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ili watoe kilio chao.
TABOA
iliomba kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao
kutokana kwa madai kuna sheria na kanuni za usalama barabarani ambazo
ni kandamizi kwao na zimekuwa zikiwaweka katika wakati mgumu katika
kutoa huduma ya kusafirisha abiria nchii.
Hata
hivyo TABOA bado hawajafanikiwa kuonana naye ingawa tayari ameshawapa
maelekezo kuwa wakati wowote atakutana nao na kisha kuwasikiliza ili
kupata muafaka kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafiri wakiwamo
Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra).
Akizungumza
na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Mrutu amesema wanatambua
majukumu aliyonayo Waziri Mkuu hivyo wana imani akipata muda watakutana
naye na kisha kuzungumza kwa kina kuhusu changamoto ambazo wanakabiliana
nazo watoa huduma ya usafiri nchini.
"Ombi
letu kwa wanachama wa Taboa waendelee kutoa huduma bora ikiwa pamoja na
kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali.Tunamatumaini makubwa na Waziri
Mkuu, hivyo tunajua akipata muda atatuita ,nasi tupo tunasubiri.Hivyo
wakati tunaendelea kumsubiri tuendelee kutoa huduma ya usafiri bila
kuchoka,"amesema Mrutu.
Taarifa
za awali ambazo Michuzi Blog ilizipata ni kwamba Taboa walitaliwa
kukutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita lakini
hawakufanikiwa kukutana naye kutokana na majukumu aliyonayo, hivyo
aliwahakikisha atapanga ratiba ya kukutana nao.
Hata
hivyo kwa muda mrefu sasa Taboa na Sumatra wamekuwa katika mvutano wa
hapa na pale uliosababisha Chama hicho kutishia kutotoa huduma kwa madai
ya kutoridhishwa na faini kuanzia Sh 200,000 hadi Sh 500,000
zinazotozwa kwa mabasi hayo pindi yawapo safarini.
Taboa
kupitia kwa Mrutu amesema wanasikitishwa na faini hizo ambazo kibaya
zaidi hata wakati wa mchakato wa kuziandaa Sumatra hawakuwashirikisha
wadau wa usafirishaji wakiwamo wao na hivyo kuibua malalamiko.
"Mbali
ya kutoshirikishwa wakati wa mchakato wa uandaaji wa faini hizo, pia
utaratibu wa faini hizo unakiukwa kwa kuwahusisha wamiliki hata katika
makossa yanayowahusu madereva.Pamoja na malalamiko yetu tunaendelea
kuwahamisha wanachama wetu waendelee kutoa huduma iliyobora kwa manufaa
ya nchi yetu,"amesema.
Wakati
huo huo TABOA imesema imesikitishwa na ajali ya basi iliyotokea mkoani
Kigoma na kusababisha abiria 10 kupoteza maisha na madereva kuwa makini
ili kuepuka ajali za barabarani.
No comments:
Post a Comment