Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mst. Thomas
Mihayo (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.
Hamisi Kigwangalla kuhusu Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya
Karibu/Kili Fair 2018 kabla ya kuzindua maonesho hayo katika uwanja wa
Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Nape Nnauye (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi
Warioba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilifair Promotion,
Tom Kunkler (kushoto).
Na Hamza Temba-WMU-Moshi
.............................. .............................. ...........
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa taasisi
za Serikali, jamii, sekta binafsi na wadau kwa pamoja kushirikiana
kuendeleza utalii katika maeneo yao ili sekta hiyo iweze kunufaisha
zaidi taifa kwa kiwango kinachostahiki kuliko ilivyo hivi sasa.
Ametoa
wito huo juzi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi
wakati akifungua maonesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu/Kili Fair
2018 ambayo yameshirikisha makampuni na wadau wa utalii zaidi ya 350
kutoka nchi zaidi ya 12 duniani huku na kuvutia watu zaidi ya 4,000
kuyatembelea.
Amesema
ushirikiano huo utaiwezesha sekta hiyo kuongeza mchango wake katika
uchumi wa Taifa ambao kwa sasa ni takriban asilimia 17.2 ya pato la
Taifa, zaidi ya asilimia 24 ya mapato yote ya fedha za kigeni sambamba
na zaidi ya asilimia 10 ya ajira zote nchini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijaribu kuendesha
baiskeli maalum ambayo hutumika kwenye utalii wa baiskeli kwenye maeneo
mbalimbali ya hifadhi nchini baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya
Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha
Ushirika mjini Moshi.
Kutoka
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce
Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Devotha Mdachi
wakiwa katika meza kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kabla ya kuzindua Maonesho ya
Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu
cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd,Tom Kunkler,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mkurugenzi wa Karibu Fair,
Dominick Shoo na
viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye picha ya
pamoja baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili
Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Nape Nnauye kwenye eneo la mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima
Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya
Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini
Moshi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na
viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye eneo la
mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima Kilimanjaro baada ya kuzindua
Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja
wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Waziri Kigwangalla akisalimia baadhi waoneshaji katika banda la utalii wa kiutamaduni kwenye maonesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiangalia moja ya gari la kitalii la wazi katika maonesho hayo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya gari
maalum la kusafirisha watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni
ya Hanspaul Automechs Ltd ya Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya
Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo
Kikuu cha Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni hiyo, Satbir Singh Hanspaul.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo
la Mtama, Nape Nnauye (kulia) kwenye moja gari maalum la kifahari la
kusafirisha watalii ambalo limebuniwa hapa nchini na kampuni ya Hanspaul
Automechs Ltd ya Jijini Arusha baada ya kufungua Maonesho ya Utalii ya
Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha
Ushirika mjini Moshi.
Waziri Kigwangalla akipanda gari maalum la kusafirisha watalii katika maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa wizara hiyo, Deogratious Mdamu wakiwa
ndani ya gari hilo maalum la kusafirisha watalii kwenye maonyesho hayo.
Waziri Kigwangalla akiwa amejilaza kwenye moja ya kitanda maalum katika hema la kitalii katika maonesho hayo.
Waziri
Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini,
Jorg Herera katika moja ya chumba maalum cha wazi cha kitalii katika
maonesho hayo.
Waziri
Kigwangalla, Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Jorg Herera na
viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye chumba hicho cha wazi cha
kitalii katika maonesho hayo.
Waziri
Kigwangalla akiwa kwenye banda la Bodi ya Utalii na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini wa bodi hiyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kushoto),
Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi (wa pili kushoto), wafanyakazi
wa bodi hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Promotion Tom Kunkler.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki kupekecha
mti maalum uliokuwa ukitumika enzi za mababu kwa ajili ya kufua moto
katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018
yanayoendelea katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la
Mtama, Nape Nnauye (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Longido, Dkt. Steven
Kiruswa (wa pili kulia) wakishiriki kucheza ngoma za kimasai na kikundi
cha ngoma cha kabila hilo baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya
Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha
Ushirika mjini Moshi.
No comments:
Post a Comment