Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Makoye Alex
Nkenyenge akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (Hayupo katika picha) wakati
wa ufunguzi wa kikao cha13 cha Baraza la
Wafanyakazi kilichofanyika leo Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi za Waziri
Mkuu
Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa kufarijiana Bw.
Mussa Varisanga akiwasilisha taarifa kuhusu mfuko huo wakati wa kikao cha 13
cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
,kilichofanyika leo Mkoani Dodoma.
Afisa Ushirika kutoka
Manispaa ya Dodoma Bw.Greyson Masawe akiwasilisha mada kuhusu uanzishaji wa
Chama cha Kuweka na Kukopa Akiba (SACCOSS) katika kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi la
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kilichofanyika leo Mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza
uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali wkatika kikao cha 13 cha Baraza
hilo.
Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza
uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali katika kikao cha 13 cha Baraza
hilo.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo baada ya kufungua rasmi
kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi
lkilichofanyika leo Mkoani Dodoma, (Picha na Lorietha Laurence, Dodoma).
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13
cha Baraza la Wafanyakazi lililofanyika
katika Ukumbi wa Waziri Mkuu leo Mkoani Dodoma.
Na Anitha Jonas – WHUSM,Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kuwahudumia wananchi kwa kujibu hoja na kutatua kero zao kwa haraka na ufanisi.
Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma na Waziri Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akifungua kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo, ambacho hufanyika mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za watumishi.
“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa kazi zetu” amesema Dkt. Mwakyembe. Aidha Dkt. Mwakyembe ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao ili kuimarisha utendaji wa kazi.
“Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha taratibu za kiutendaji zinafuatwa na kuzingatiwa” amesema Dkt. Mwakyembe. Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia kikao hicho ambacho kipo kwa mujibu wa sheria, na kuwasisitiza watumishi kuyafanyia kazi yale yote waliyoelezwa.
“Nawaomba watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira” amesema Bibi.Susan.
Naye Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw.Makoye Alex Nkenyenge alimshukuru mgeni rasmi kwa niaba ya wajumbe wote na kuhaidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment