Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege amewataka wauzaji,
waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini
kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule
‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote
Tanzania.
Kandege
ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa ‘Vendors
Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na
wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu
uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.
Amesema
“mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo
vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango
pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya
ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za
Afya”.
Sasa
basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo
na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato
wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo
kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.
Wakati
huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali
imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na
inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa
katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na
kurahisha mchakato wa malipo.
“Hivyo
niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka
zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika
kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana
kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.
Alimalizia
kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani
kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata
Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani
mkubwa.
Mkurugenzi
wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe amesema hivi sasa
wako katika uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya kwa kuzingatia kuwa
Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bil 31 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia
Bil 269 kwa mwaka 2017/18 hivyo ongezeko hili la bajeti linatakiwa
kwenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa na zenye ubora chini
ya usimamizi makini wa wataalamu wa Afya.
Dr.
Ntuli alisema mpango huu utaleta manufaa kwa wananchi wote ambao
watakua chini ya mpango wa Tele kwa Tele na wale wanaopata huduma
kupitia mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa; Tunataka kila mmoja apate
dawa anayoihitaji kwa wakati.
Naye
Mfamasia toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard alisema mfumo wa
Mshitiri Mteule umeanzishwa kwa sababu ya changamoto zilizoonekana awali
za kutumia mzabuni kama vile taratibu za manunuzi kuchukua muda mrefu
na gharama za manunuzi kuwa kubwa na zinazotofautiana kati ya
Halmashauri moja na nyingine ndani ya Mkoa mmoja.
Changamoto
zingine alizozibainisha ni kubadilika kwa bei mara kwa mara kila
manunuzi yanapofanyika, kutokuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa kutokana
na kuhifadhiwa na kusafirishwa katika mazingira mbayo si salama na zaidi
baadhi ya wazabuni na watumishi kutokuwa waaminifu.
Matumizi
ya mfumo huu umeelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Sera ya
Afya ya Taifa ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya
Mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Kikao
hiki cha wadau wa dawa ‘Vendor Forum’ kimefanyika kwa mara ya kwanza na
kimehusisha wadau kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele)
akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika
Ukumbi wa Dodoma Hotel.
Mkurugenzi
wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi, Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya
awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya
Vendor Forum.
Mfamasia
Mwandamizi toka Ofisi ya Rais Tamisemi, Regina Richard akielezea
malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika
ukumbi wa Dodoma Hotel mapema.
Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele katikati)
katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.
No comments:
Post a Comment