Aziz
Rashid wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom wilayani Mbulu akimiliki mpira
huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya
wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi
Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom, Timu ya Rema 1000 FC imeifunga timu
ya Airport Magoli 8-4 na kutinga fainali ambapo sasa itakutana na timu
ya Dongobesh FC ambayo nayo imeshinda mchezo wake wa leo wa Nusu Fainali
baada ya kuifunga timu ya Young Boys FC magoli 2-0 .
Mashindano
hayo yanaandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw.
Hudson Kamoga na yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom
kwa udhamini mkubwa wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mkoani Iringa na
Benki ya CRDB.
Mchezo
wa Fainali utafanyika kesho kwenye uwanja wa huohuo kwa kuzikutanisha
timu za Dongobesh FC na Rema 1000 FC ambapo pia kutakuwa na burudani
mbalimbali za ngoma za asili wakiwemo pia wachekeshaji MC Pilipili na
Katarina wa Karatu.
Aziz
Rashid wa Rema 1000 FC ya Haydom Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma
Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya huku kiatu kikiwa
kimechomoka mguuni wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya
Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom
Kocha
wa timu ya Rema 1000 FC Bw. Jared Ochieng akiwaelekeza wachezaji wa timu
yake kwa kuchora chini kutokana na makosa waliyokuwa wakisababisha
katika mchezo huo wakati wa mapumziko.
Bw.Samson
Madawabora ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Haydom na mmiliki wa
timu hiyo akiwapongeza wachezaji wake mara baada ya kutinga fainali ya
michuano hiyo leo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya
viongozi wa halmashauri hiyo wakifuatilia mchezo huo.
Wachezaji
wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakisalimiana kabla ya kuanza
kwa mchezo wao wa pili wa nusu fainali uliochezwa leo kwenye uwanja wa
shule ya Msingi Haydom.
Kikosi cha timu ya Young Boys FC kikiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji
wa timu ya Dongobesh FC na Young Boys FC wakichuana vikali katika
mchezo wao wa nusu fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi
Haydom leo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga kulia akiwa na
Mchekeshaji MC Pilipili wakifuatilia mchezo wa Nusu fainali kati ya timu
ya Dongobesh FC na Young Boys FC.
Mchekeshaji
MC Pilipili akitangaza mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya Dongobesh
FC na Young Boys FC wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa shule
ya Msingi Haydom.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akiwa na mtangazaji
wa Radio Clouds Jacob Mbuya wakishuhudia mchezo huo.
Mashabiki
wa timu ya Dongobesh FC wakimbeba juu juu golikipa wao anayejulikana
kwa jina la Mapilau mara baada ya kuibuka washindi wa mchezo huo na
kutinga fainali.
Mashabiki mbalimbali wakiwemo akina mama wakiwa wamefurika uwanjani kushuhudia mchezo huo.
No comments:
Post a Comment