Waziri
wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya
Siasa kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama
vya siasa.
Ametoa
kauli hiyo Aprili 23, 2018 alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya
hoja za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018
alipokutana na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Waziri
Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu
zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.
“Namtaka
Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama
chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka
1992”.alisema Waziri Mhagama
Aidha
amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo
na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache
mara moja kwa mujibu wa sheria.
Waziri
Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya
siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango
vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya
vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi
Pamoja
na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista
ya mali za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na
Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume
na sheria zilizopo.
“Msajili
wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa kila chama cha siasa chenye
usajili wa kudumu kuwa na regista ya mali zake ndani ya wiki tatu
kuanzia kwani kukosa daftari la mali za kudumu ni kinyume na kifungu
Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya mwaka
1992.”alisisitiza Waziri.
Sambamba
na hilo Waziri alimtaka Msajili wa Vyama vya siasa kuhakikisha vyama
vyote vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili kuondokana na mapungufu
ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu
wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama vitatu kati ya tisa vina
nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.
“Msajili
wa vyama ahakikishe vyama vya siasa vinatekeleza miongozo yote kihasibu
pamoja na kanuni za fedha, ambazo zinaelekeza nyaraka ziwe na
viambatisho sahihi kwani ripoti ilibainisha vyama vitatu vilikuwa na
malipo yenye nyaraka pungufu zenye thamani ya shilingi 735,978,559
ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa uhalali wa malipo
hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.
AWALI:
Kifungu
cha 14(1)(a) na (b)(i) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE:
2015] kinaelekeza kuwa, kila chama cha siasa kinapaswa kutunza taarifa
za mapato na matumizi, ikiwamo taarifa za mali zake. Vile vile,
kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, taarifa ya hesabu
zake zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), pamoja taarifa ya mali zake.
Hivyo,
Kifungu hicho kinampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kufanya ukaguzi wa hesabu za kila chama cha siasa chenye
usajili wa kudumu. Katika mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2017,
CAG amefanya ukaguzi wa hesabu za Vyama vya Siasa kumi ikiwemo; CCM,
CHADEMA, NLD, TLP, Demokrasia Makini (MAKINI), TLP, DP, SAU, AFP, CCK na
ADC kati ya vyama vya siasa kumi na tisa vyenye usajili wa kudumu.
Vyama vya Siasa tisa (9) havikuwasilisha hesabu zake kwake kwa wakati
kwa ajili ya ukaguzi, hivyo hakukaguliwa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari
juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya
Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha
unoishia Juni 30, 2018 Bungeni Dodoma.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Idara ya
Habari Maelezo, Kwa Mawaziri walipokutana kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya
hoja zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa mkutano na
waandishi wa habari Dodoma Aprili 23, 2018.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment