Na Anthony Ishengoma WAMJW
Msajili
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs Marcel Katemba amewataka
Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzisimamia
NGOs ili zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.
Ameyasema
hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Wasajili Wasaidizi
ili kutoka mafunzo kwa ajili ya kukumbashana majukumu yao Kama wasajili
wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Amesema
kuwa kimsingi Mashirika yasiyo ya Kiserikali bado hayatambui umuhimu
wenu hivyo tutawakutanisha na Mashirika haya kwa ajili kufahamiana
kiutendaji na kutambuana.
Aidha
Katemba amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati mwingine yanakosa
majibu muhimu kutoka kwa Wasajili Wasaidizi hivyo kusababisha waone
kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii sio watu sahihi kusimamia shughuli zao.
"Lengo
la Mafunzo haya nikukumbashana mambo muhimu ambayo yatawafanya muweze
kutoa majibu stahiki kwa Mashirika haya na kuyasimamia ipasavyo baada ya
kujua shughuli wanazozifanya"alisisitiza Bw. Katemba.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya NGOs ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Baraka Leornard amewaambia wajumbe wa
mafunzo haya kutoka Halmashauri zote kuzisimamia NGOs ili ziweze
kuhudumia Wananchi.
Bwana
Baraka ameongeza kuwa kimsingi mafunzo haya ni ya kuwajengea uwezo
wasajili wasaidizi wa serikali ili waweze kujua utaratibu wa kusajili na
kuyasimamia Mashirika haya kwa matumizi mazuri ya fedha za umma
wanazopata kupitia wafadhili wao.
"Pamoja
na Masharika yasiyo ya Kiserikali kupata fedha kutoka kwa wafadhili ni
muhimu wakatambua fedha hizo ni mali ya umma na ninyi wasajili wasaidizi
mnayo haki yakujua matumizi ya fedha hizo".Alisisitiza Bw. Baraka.
Mafunzo
kama haya yamekuwa yanatolewa nchi nzima na Msajili wa Mashirika yasiyo
ya Kiserikali kwa Wasajili Wasaidizi wa Mashirika haya ambao ni
maafisa Maendeleo wa Jamii wa Halmashauri za Wilaya hapa Nchini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo
Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo
ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es
Salaam katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya
uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
Baadhi
ya Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Dar es
Salaam wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na
Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha kujadili namna
bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi
Msaidizi Usajili wa NGOs Bw. Baraka Leonard na Mkurugenzi Msaidizi
Ufuatiliaji Bi. Tausi Malima wakijadiliana jambo wakati wa kikao kazi
kati ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili wasaidizi
wa Mashirika hayo mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa
Karimjee kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika
hayo mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka
akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na
baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa Wasajili wasaidizi wa
Mashirika hayo kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam
katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee
kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani
humo.
Mkurugenzi
Msaidizi Ufuatiliaji NGOs Bi. Tausi Malima akizungumza na Maafisa
Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam na
wasajili wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kuhusu
umuhimu wa ufuatiliaji wa ufanyaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali baada ya kupata usajili wake katika kikao kilichowakutanisha
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili Wasaidizi
kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee kilicholenga kuboresha namna
bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
Afisa
Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali katika Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana(kushoto)akiomba
ufafanuzi zaidi kuhusu masuala yahusuyo Usajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali na Wasajili Wasaidizi hao mkoani Dar es Salaam
kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee kilicholenga kuboresha
uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani
humo.
Afisa
Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Given Sure(kulia) akiuliza
swali kuhusu masuala yahusuyo Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika
kikao kilichowakutanisha na Msajili wa NGOs na Wasajili Wasaidizi mkoani
Dar es Salaam kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa
kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo. Picha na Kitengo cha
Mawasiliano WAMJW
No comments:
Post a Comment