Na Mwandishi wetu
Washiriki
wa mafunzo ya ufundi mitambo ya kurushia matangazo ya redio ambayo
yameshirikisha mafundi kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na
Zanzibar wametakiwa kutumia vyema mafunzo ili yakalete mabadiliko katika
maeneo yao ya kazi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC), Mwandisi Upendo Mbele wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo
ya siku saba ambayo yameandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mbele
alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatawapa uwezo wa kujua vifaa
ambavyo wanavitumia katika vituo vyao na hivyo ni vyema wakayatumia
vizuri ili yalete mabadiliko katika maeneo ya kazi.
"Ukiwa
fundi mafunzo ni lazima, tuwashukuru UNESCO kuandaa mafunzo haya na
nyie mtumieni muda wenu vizuri mkiwa hapa. Lengo kuu la kuwa hapa ni
kujenga na kuboresha kile kitu ambacho hakikuwepo, unavyokuwa na upana
zaidi na wewe utakuja kuwa mwalimu kwa wengine," alisema Mbele na
kuongeza.
"Mkikaa
pamoja tunaamini mtabadilishana ujuzi kuhusu mambo mbalimbali, lakini
kama mkifika na mkawa mnatumia tu mitandao mtatoka kama mlivyoingia.
Tumeambiwa kuwa tutakuja kuangalia kwenye vituo vyenu kama mafunzo
mnayopewa hapa mnaelewa, maana isije mkatoka hapa alafu mkarudi kule
mkawa mnafanya tofauti."
Naye
mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni fundi na mwandishi wa
habari wa redio Kahama FM, Bakari Khaled alisema ni mambo mengi
wamejifunza katika mafunzo hayo ambayo kwa namna moja au nyingine
yatawasaidia kutatua matatizo ya ufundi ambayo yanawakabili.
"Tumekuwa
tukinufaika na mafunzo haya, yametusaidia sana, redio jamii nyingi
hazina uwezo wa kuajiri mafundi kabisa katika vituo na badala yake wana
mafundi ambao wanawatumia kunapotokea tatizo, lakini kwa sisi ambao
tumepata uzoefu na ujuzi huu matatizo madogo ambayo yanatokea
tunayafanya wenyewe,
"UNESCO
wamekuwa wakitusaidia sana, kwa sasa redio jamii zimetoka katika hatua
ya chini na sasa zimekua hata kushindana na redio zengine za kibiashara,
na TBC wamekuwa wakitufunza mambo mengi sana kwahiyo tukienda kujifunza
pale tunaona kwa macho kwamba hiki kilitumika wakati wa analog na hiki
ni digital, mafunzo haya yametujenga sana," alisema Khaled.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mwandisi
Upendo Mbele wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya ufundi mitambo ya kurushia
matangazo ya redio kwa mafundi mitambo wa redio jamii 25 kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar ambayo yameandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya ufundi mitambo ya kurushia matangazo ya
redio kwa mafundi mitambo wa redio jamii 25 kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar ambayo yameandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Washiriki
wa mafunzo ya ufundi wa kurushia matangazo ya redio kwa mafundi mitambo
wa redio jamii 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakipewa maelezo
kuhusu matumizi ya mitambo hiyo.
No comments:
Post a Comment