Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akifafanua jambo jana wakati
wa kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali
za barabarani mkoani humo kichofanyika jana Wilayani Igunga na
kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora na ile ya
Wilaya ya Igunga na wadau mbalimbali wa usafiri. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Igunga John Mwaipopo na kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
Wilbroad Mtafungwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye na kofia ya kijani) akiwa kwenye
ilipotokea ajali ya Basi la City Boy kugonagana uso kwa uso na lori siku
ya Jumatano usiku.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiliangalia Basi la City Boy lilopata
ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara
baada kuongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ile ya Wilaya
ya Igunga kutembelea eneo la tukio.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye kofia ya kijani) na Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga wakiliangalia Basi la
City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya
Jumatano usiku.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwafariji majeruhi wa ajali ya Basi la
City Boy iliyogongana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara
baada kutoka katika ilipotokea ajali wilayani Igunga
……………….
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
KAMATI
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadau wa Usafiri
wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu(log book) kwa magari ya
mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na
hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na
magari mengine kutokana na uchovu.
Tamko
hilo limetolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri mara baada ya kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu
ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo vitasaidia kuonyesha muda alitoka ,
mahali alitoka na kama amesafiri muda mrefu atalazimisha apumzike ili
kuepusha ajali.
Alisema
malori yamekuwa yakisafiri mwendo mrefu bila hata dereva wake kupumzika
jambo ambalo limesababisha magari hayo yapate ajali au wakati mwingine
yawe chanzo kinachosabisha ajali katika magari ya abiria.
Mwanri
alisema kwa kulitambua hilo wanaona wakati umefika kwa magari ya mizigo
nayo kuwa na vitabu(log book ) inayoonyesha muda alianza safari katika
kituo chake cha kwanza na muda alipo baada ya kusimamishwa ili kuona
kama kweli amezingatia matawaka ya kitaalamu na sharia ya kutokwenda
kasi.
Alisema
kitaalamu dereva anatakiwa aendeshe chombo cha moto kwa muda usiozidi
saa nane lakini mara nyingi madreva wa malori wamekuwa wakiendesha
magari yao hata zaidi ya muda huo jambo ambalo limekuwa kiwasababisha
baadhi yao kuendesha huko wakisinzia na kupelelea gari kukosa mwelekeo.
Mwanri
alisema ili kuepukana na hilo wadau wamependekeza wammiliki wa gari wa
ya mizigo ya masafa marefu ni vema wawe na madereva wawili ili
wasaidiane.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema hatua nyingine ambayo wameamua kuichukua ni pamoja
na kuongeza askari na magari ya doria katika barabara kuu ya Igunga,
Nzega kwenda Mwanza na Shinyanga.
Alisema
hatua hii inalenga kupambana na madreva ambao nyakati za usiku wakwenda
mwendo mkali kwa sababu ya kujua kuwa nyakati hizo tochi hazifanyi
kazi.
Mwanri
aliongeza kuwa Wadau wa usafiri wameiagiza Wakala wa Barabara
Tanzania(TANROADS) mkoani Tabora kuhakikisha wanaziba mashimo yaliypo
katika barabara kuu zote ili kuondoa uwezekano wa yenyewe kuwa chanzo
cha ajali za barabarani.
Aidha
alisema kuwa Wadau wamekuwabaliana kuwa ukaguzi wa madereva na magari
katika barabara kuu zinazopita Mkoani Tabora utakuwa unafanyika kila
siku ili kujihakikishia kama gari linazo breki, taa zifanya kazi vizuri ,
matari yako vizuri na dreva ajatumia kilevi.
Alisema hatua hiyo inalenga kujihakikishia kama chombo cha usafiri na dreva wake yuko katika hali nzuri.
Hivi
karibuni (4 /4/2018) kulitokea ajali ambapo basi la abiria Kampuni ya
City Boy yenye namba T 983 DCE iligongana uso kwa uso lori lenye namba T
.486 ARB Mitsubishi Fuso wilayani Igunga na kusababisha watu 12 kufa
palepale na mmoja kufia katika Hospitali ya Rufaa Bugango.
Taarifa
za awali zinaoonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa
dereva wa Fuso uliosababisha tairi kupasuka na gari kuhamia upande wa
basi.
Lori hiyo lilikuwa na viazi ambavyo lilivitoa Njombe Mwisho
No comments:
Post a Comment