SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limeanza
kutoa mafunzo ya siku saba kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Shirika hilo jijini Dar es
salaam, mafunzo hayo yanagusa masuala yanayozunguka jamii namna ya
kuyafanya kifanisi na kitaalamu ili kuweza kurusha matangazo
yaliyomazuri kwa jamii ambayo yameanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka
huu.
"Washiriki
hawa wanatoka katika radio 25 za jamii zinazosaidiwa na shirika
letu.Kubwa ni kuwapa mafundi mitambo hao elimu kuhusu namna ya kuifanya
radio ya jamii kuwa bora wakati wa urushwaji wa matangazo kwa jamii
husika,"imesema.
Imeongeza
Unesco kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) husaidia
radio za jamii na mtandao wa radio za jamii (TADIO).
Ufadhili
huo umelenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania hasa wale wa vijijini
wanafanya uamuzi sahihi kuhusu maisha yao kwa kupata taarifa sahihi
kutoka redioni.
Washiriki
wanaofadhiliwa na SDC ni Nuru FM (Iringa), Pambazuko FM (Morogoro),
Fadhila FM (Mtwara) Jamii Mtukwao FM (Mtwara), Loliondo FM (Arusha),
Baloha FM (Shinyanga), Kahama FM (Shinyanga) Ileje FM (Songwe),Tripple A
FM (Arusha) na Storm FM (Geita).
Pia
Sengerema FM (Mwanza), Kwizera FM (Kagera), Dodoma FM (Dodoma), Kitulo
FM (Njombe), Uvinza (Kigoma), Mpanda (Katavi), Pangani (Tanga), Boma
(Kilimanjaro), Mazingira (Mara), Mtegani FM (Kusini Unguja),mkoani FM
(Kusini Pemba), Micheweni FM (Kaskazini Pemba),Tumbatu FM (Kaskazini
Unguja) na Ruangwa FM (Lindi).
Afisa
Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Rose Ngunangwa akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
Meneja
wa Huduma za Ufundi kutoka TBC, Mhandisi Yusuph Afidhu akizungumza na
washiriki kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za
jamii zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkuu
wa Studio Redio ya TBC, Mhandisi Omary Salum akitoa mada kuhusu namna
ya studio inavyobidi kuwa ili kuweza kurusha matangazo kistadi wakati wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
Baadhi
ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakifuatilia mada kwenye mafunzo
ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25
yaliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakichangia mada kwenye mafunzo ya
kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment