Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wakwanza
kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya
Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayumo pichani) kuhusu mpango
kazi wa kuboresha uwekezaji Tanzania. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana anayeshughulikia
Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila.
Mkurugenzi
Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe
(kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), (hayumo pichani) wakati wa majadiliano ya
namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania, kushoto kwake
ni Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw, Zarau Kibwe.
Picha
ya pamoja ya wajumbe walioshiriki majadiliano ya Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji
Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe kuhusu
uboreshaji wa sekta binafsi, miradi ya maendeleo, ukuaji wa uchumi
pamoja na sekta ya ukuaji wa viwanda. Wanaopeana mikono kulia Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)kushoto Mkurugenzi
Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe.
Kutoka kulia ni Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt.
Yamungu Kayandabila, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw.
Charles Kichere, wa pili kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
Prof. Florens Luoga na wa pili kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji
Mbadala Benki ya Dunia, kanda ya Afrika Bw, Zarau Kibwe.
………………
Na. WFM- Washngton DC
Mikutano
ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki
ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika
mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi
pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili hali ya uchumi wa dunia
pamoja na kupunguza umasikini.
Katika
mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia,
Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa
Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali
ya uchumi wetu kwa nguvu zote.
Akiendelea
kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya
ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali
imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na
uwekezaji katika Taifa la Tanzania.
Pia
Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza,
ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa
Bwawa kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler’s Gorge’
katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji.
Kupitia
miradi hiyo ambayo Serikali imepanga kuifanikisha kwa wakati Dkt.
Mpango alimuomba Bw. Bvumbe kuendelea kuzungumza na uongozi wa Benki ya
Dunia ili uweze kutusaidia katika kuwezesha uwekeza katika miradi hiyo.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika
Bw. Andrew Bvumbe alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa jitihada
inazozionesha hasa katika kupambana na rushwa na ametutia moyo tuendelee
na juhudi zetu za kuimarisha uchumi wetu hususani katika sekta ya
kilimo na pia amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanya kwa ajili ya
kuendeleza sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment