Mhe. Charles
J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, akizungumza
wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika
halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili,
2018. Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA
Baadhi ya wakuu wa mikoa inoyozalisha Pamba kwa wingi wakifatilia mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Mgeni-Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Charles
J. Mwijage (Mb), akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa
wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye
ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Naibu
waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Mary Mwanjelwa akijadiliana na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya pamba
na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini
Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Waziri wa kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebawakati
akifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi
katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20
Aprili, 2018.
Baadhi ya wadau wa sekta ya pamba wakifatilia kwa
makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali
kwa kushirikiana na viwanda vya nguo na mavazi imeanzisha mpango maalum
wa kutoa mafunzo ya ushonaji kwa vijana kwa ajili ya kukidhi mahitaji
ya viwanda vya nguo.
Upatikanaji wa ujuzi wa aina hiyo utapunguza gharama kwa wawekezaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Vilevile, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, kupitia msaada wa Gatsby Africa, kimeendelea
kutoa mafunzo ya Shahada ya Teknolojia ya Nguo (Textile Degree) ambapo,
mwaka 2016/2017, Chuo kilitoa wahitimu 44 ikilinganishwa na wahitimu 13
kwa mwaka 2015/2016. Lengo ni kuhakikisha kuwa kuna wataalam wa kutosha
wa fani ya ubunifu na uzalishaji mavazi nchini.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Charles
J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, wakati
akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018
Alisema kuwa Tanzania
ni moja ya nchi zinazozalisha pamba kwa kiasi kikubwa barani Afrika,
ikiwa na zaidi ya wakulima 500,000 wanaolima pamba katika eneo
linalokadiriwa kufikia hekta 412,000 katika mikoa 13 nchini. Sekta
ya nguo na mavazi ni moja ya sekta za Kipaumbele katika kusukuma
gurudumu la maendeleo nchini na inahusisha mnyororo mrefu wa uongezaji
thamani kuanzia kuchambua pamba (ginneries); kusokota nyuzi (spinning);
kuseketa vitambaa (weaving); kufuma vitambaa (knitting),kuchapa na kutia rangi (processing) na kushona mavazi (garments).
Aliongezaa kuwa Sekta
hii ni moja ya sekta muhimu katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya
kuanzisha viwanda vinavyoajiri watu wengi kwa wakati mmoja. Sekta hii
itawezesha kupunguza uingizaji wa nguo kutoka nje na kuongeza matumizi
ya pamba inayolimwa nchini pamoja na malighafi nyingine zinazopatikana
nchini kama vile magadi na gesi asilia.
Hata hivyo, Serikali
imeendelea kuzishawishi taasisi za Umma kwa kuanzia majeshi na
hospitali ili wanunue nguo na mavazi yanayozalishwa na viwanda vya
ndani. Lengo ni kuhakikisha kuwa
utaratibu wa makusudi unawekwa kwa Taasisi za umma kutumia bidhaa
zinazozalishwa na viwanda vyetu hapa nchini. Kwa mfano uvaaji wa fulana
aina ya Polo Shirt kwa wafanyakazi wote katika siku moja ya wiki, na pia
wanafunzi wote shule za msingi na sekondari kuvaa sare hizo.
Inakadiriwa kuwa kuna jumla ya wanafunzi milioni 15 na wafanyakazi wa
sekta zote za umma wanafika 25,000.
Mhe Mwijage alisema kuwa Utengenezaji
wa fulana moja ya polo unakadiriwa kutumia wastani wa gramu 300 za
pamba, sketi moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba, kaptula moja
inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba. Hivyo jumla ya gramu 900 za
pamba zitahitajika kutengeneza sare kwa mwanafunzi mmoja awe wa kike au
wa kiume.
Kama
ikikadiriwa kila mwanafunzi atavaa wastani wa sare (sketi & shati
au kaptula na shati) mbili tu kwa mwaka gramu 1800 (sawa na kilo 1.8) za
pamba zitahitajika kwa mwanafunzi mmoja, hivyo wastani wa kilo
27,000,000 (sawa na tani 27,000) zitahitajika kwa mwaka. Endapo mahitaji
yaliyokusudiwa yakipitishwa tunategemea kwamba viwanda vya ndani
vitakuwa na uwezo wa kutumia asilimia 17 ya pamba yote inayozalishwa
nchini kwa mwaka. Hii itahamasisha uzalishaji wa pamba, kuongeza ajira
na kuongeza kipato.
“Serikali inakamilisha taratibu za kuidhinisha ‘’ Blue Print’’ ambayo
imeainisha maeneo ya kufanyia maboresho ya Kisera na Kisheria ili
kuhamasisha uwekezaji katika Sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya
pamba nguo na mavazi” Alikaririwa Mhe Mwijage
Pia,aliwashukuru
Wadau wa sekta ndogo ya pamba, nguo na Mavazi kwa kazi kubwa
wanayofanya katika uzalishaji, biashara na wadau wengine kwa michango
yao katika kuendeleza sekta hii.
Mkutano
huo umehusisha Wizari ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara wa Fedha
na Mipango, Wizara ya Kilimo; Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu
za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira; Bajeti; Kilimo, Mifugo na
Maji; na Uwekezaji Mitaji ya Umma, Wakuu wa Mikoa; Makatibu Wakuu,
Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Maafisa wa Serikali na Taasisi za
Serikali.
No comments:
Post a Comment