Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Ndunguru (wa tatu
kutoka kushoto) akiongoza wadau mbalimbali kufungua bomba wakati wa
uzinduzi wa mradi wa maji wa Mkinga mkoani Tanga.
Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi.
Mratibu
wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International
Tanzania, Isack Abdiel, akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya.
Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.
Shirika
la Kimataifa linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water
Missions International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi
mkubwa utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga
utaowawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa
matumizi yao na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi.
Kwa
kipindi cha muda mrefu wilaya ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa maji salama, kutokana na kutokuwepo na vyanzo
vya uhakika vya maji katika eneo hilo.Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni,
Mwakihonda and Karoyo vimekuwa vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka
tanki la zamani la kusambaza maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere,
ambalo limekuwa halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji
hivyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory
Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo
ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu
wilayani hapa kutawezesha wananchi kupata maji safi ya uhakika wakati
wote,kwa niaba ya serikali nalishukuru shirika la Water Missions
International Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania
ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali
nchini”.
Mhandisi
Ndunguru, alisema mradi huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi
wakazi wa Mkinga na kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia
muda wao mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia .
Alitoa
wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa shirika hilo
sambamba na kutunza miundo mbinu itakayowekwa katika maeneo yao ili
kuwezesha mradi kuwa endelevu. “Mradi huu muhimu hapa Mkinga pia
utaimarisha afya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa mbalimbali
yanayosababisha na ukosefu wa maji na matumizi ya maji yasiyo salama kwa
kuwa hivi sasa tuna uhakika wa kupata maji salama,”alisisitiza.
Kwa
upande wake,Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions
International Tanzania ,Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kuzindua
mradi wa maji katika wilaya ya Mkinga ,ukiwa ni mwendelezo wetu wa
kuunga mkono serikali ya Tanzania kuboresha upatikanaji wa maji ya
uhakika na salama kwenye jamii zenye upungufu wa maji nchini,tunayo
imani wananchi mmeupokea vizuri na mtaulinda ili uwe mradi endelevu ili
unufaishe mpaka vizazi vijavyo”.
Aliwashukuru
watendaji wa serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali inayoshirikiana
nayo na wadau wote ambao wamefanikisha jitihada za kuanzisha mradi huu
wilayani Mkinga. Shirika la Water Missions International
Tanzania,lilianza kufanya kazi nchini mnamo mwaka 2013, likiwa
limejikita katika kuendesha miradi ya kuondoa kero ya maji kwenye jamii
,sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi ya maji.Hadi
kufikia sasa shirika limefanikisha miradi ya maji katika mikoa zaidi ya 6
nchini,ikiwemo mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Kagera na Tanga.
Ofisi
za makao makuu ya Water Missions International Tanzania nchini yapo
jijini Dar es alaam na ndipo inaporatibiwa miradi yote ya maji
inayoendeshwa na shirika nchini .Tanzania ni nchi ya 10 kuwa na miradi
ya shirika hili.Baadhi ya nchi nyingine linapoendesha miradi ya maji ni
Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, na Belize.
No comments:
Post a Comment