Na Teresia Mhagama
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amesema kuwa, baada ya miezi mitatu
Serikali itatoa uamuzi kama nchi iendelee kutumia mita za umeme
zinazotengenezwa nje ya nchi au kupiga marufuku uingizaji wa mita hizo
baada ya kujiridhisha na uwezo wa viwanda vya ndani katika kuzalisha
mita husika.
Dkt.
Kalemani ameyasema hayo jijini Dar es Salam tarehe 23 Machi, 2018
wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Baobab Energy Systems
kinachozalisha mita za umeme lengo likiwa ni kujiridhisha na uwezo wa
kiwanda hicho katika kukidhi mahitaji ya mita nchini.
"Serikali
imeweka miezi mitatu ya matazamio ili kuona kama viwanda vyetu ambavyo
sasa ni viwili, vina uwezo wa kuzalisha mita za umeme za kutosha na
zenye ubora zitakazokidhi soko la ndani kisha tutatoa uamuzi kuhusu
uingizaji wa mita hizo nchini," alisema Dkt. Kalemani.
"
Miezi kadhaa iliyopita Serikali ilitoa katazo la kuagiza nguzo za umeme
na transfoma kutoka nje ya nchi, baada ya kujiridhisha kuwa uwezo wa
kuzalisha vifaa hivyo tunao. Sasa katika mita hizi za umeme pia
tunafanya ukaguzi ili kujiridhisha na uwezo wetu," aliongeza Dkt
Kalemani.
Alisema
kuwa, uzalishaji wa vifaa vya umeme nchini una faida mbalimbali ikiwemo
kupungua kwa gharama za usafirishaji, mita kupatikana kwa haraka, kwa
gharama nafuu na kwa wingi.
"
Mfano gharama ya mita moja ya njia moja ya umeme (single phase) kutoka
nje ya nchi ni shilingi 150,000 na njia Tatu za umeme (three phase) ni
mpaka shilingi Laki Saba lakini mita zinazozalishwa nchini unazipata si
kwa zaidi ya shilingi 120,000 kwa mita za njia moja ya umeme na haizidi
shilingi Laki Nne na Nusu kwa mita za njia Tatu za umeme," alisema.
Awali
Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Baobab, Hashim Ibrahim, alimweleza Dkt
Kalemani kuwa kiwanda hicho kina unawezo wa kuzalisha mita 38,000 kwa
mwezi na kwa mwaka wanazalisha mita 456,000.
Aliongeza
kuwa, mita hizo zina faida mbalimbali ikiwemo kuwa na mfumo wenye uwezo
wa kuzuia matukio ya wizi wa umeme kwa asilimia 99 na kudhibiti upotevu
wa umeme.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, ambaye ni
Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa Shirika hilo, Theodory Bayona,
alisema kuwa mahitaji ya Shirika hilo ni mita 20,000 kwa mwezi ambapo
kati ya hizo, takriban mita 1000 ni za njia tatu za umeme. Kiasi hicho
cha mita ni kwa ajili ya wateja wapya.
Aliongeza
kuwa, mahitaji ya mita za umeme bado ni makubwa kwani kuna miradi ya
usambazaji umeme bado inaendelea nchini na pia kazi ya ubadilishaji wa
mita za zamani bado inaendelea.
Alitumia
fursa hiyo kutoa wito kwa wazalishaji wa vifaa vya umeme nchini
kuzalisha vifaa vyenye ubora pamoja na kutoviuza vifaa hivyo kwa gharama
ya juu kwani vinazalishwa hapahapa nchini.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia) akizungumza na
watendaji wa Kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za
umeme nchini . Katikati ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hashim Ibrahim.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza mara baada ya kufika katika
kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme nchini.
Wengine katika picha ni watendaji wa kiwanda hicho, Wizara ya Nishati,
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
za
umeme katika kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za
umeme nchini. Wengine katika picha ni watendaji wa kiwanda hicho, Wizara
ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hashim
Ibrahim na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi
Amos Maganga.
No comments:
Post a Comment