WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi
pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo
Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi
yao
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza
mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana
matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
WAZIRI
wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la
Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali
ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.
Hayo
ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinachow asaidiawaat hirika wa
madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo
alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.Waziri
Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono
na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya
matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.
Alisema
nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola
kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze
kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.“Jambo
linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama
serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi
mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.
Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo lakutosha
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo
cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote
wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.
“Jamani
hawa watu wasiishi kw a kuombaomba lazima wapatiwe eneo lao na
waanzishe miradi yao itakayowasaidia kujikimu na mahitaji ya kila sikuna
tukifanya hivi tutaokoa kundi kubwa la vijana linaloangamia sikihadi
siku”Alisema Waziri Ummy.Mbali
na hilo alisema akiwa kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha dawa za
Methadol zinafika Moani hapa kama ilivyo katika mikoa mingine ili kuweza
kuwasaidia vijana hao kupunguza makali ya madawa.
“Kwanza
nashangaa kama tanga haipati dawa hizi za methadol ikiwa ni mkoa wa
pili baada ya dare s salaam kwa wingi wa watumiaji wa mada ninayo dhaama
na dawa hazi zitafika sasa kwa ajili ya vijanawetu”Alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Said Bandawe alisema kwasasa
wanaishi katika nyumba ya kupanga na wamepewa eneo na wamepewa eneo la
mtu kwa kuazimwa kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga nashughuli za
ufugaji.
Alisema
maisha ya vijana bado magumu hasa swala la chakula,malazi,dawa za
Methadol, na namna ya kupata mahitaji ya kila siku kwa ujumla huku
akijaribu kutafuta mahitaji kwa kuomba misaada kuwasaidia vijana
haowanaokadiriwa kufikia 68 (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment