Meneja
Matekelezo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena,
(kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango
leo Agosti 31, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MUITIKIO
wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa
Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja
Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.
Itakumbukwa
ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa
hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha
michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.
“Kwakweli
tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa
msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa
kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema
Bw. Luvena
K-VIS
Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti
31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la
Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF kujisajili na
kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa
na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.
Afisa
Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti
cha usajili Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya
jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
Afisa
Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, akimsikiliza Mwajiri
huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
Afisa
Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto),
akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
Afisa
Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw.
Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es
Salaam.
Meneja
Matekelezo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena,
(kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika leo Agosti 31, 2017 ili
kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.
Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.
















Post a Comment