Na Bashir Yakub.
1. WAHUSIKA
Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza.
Walalamikiwa(respondents)
ni watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti
wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai
Kenyatta.
Pia
kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza
mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa
mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law
Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama.
Wa
tatu na nne ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia
kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa
wagombea urais.
2. MUDA WA KESI.
Kwa
katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea
siku matokeo yalipotangazwa. Na mahakama inazo siku 14 tu za kusikiliza
na kutoa hukumu tokea siku shauri lilipofunguliwa.
Kesi
hii imekuwa ikisikilizwa mpaka usiku saa tano zikiwemo siku za
jumamosi na jumapili ili kuendana na muda wa katiba.
3. MAHAKAMA NA MAJAJI.
Mahakama inayosikiliza ni mahakama ya juu( the supreme court).
Majaji
wanaosikiliza ni 7 wakiomgozwa na Jaji mkuu David Maraga na naibu wake
mwanamama Philomena Mwilu. Wengine ni Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim,
Njoki Ndung'u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.
4. HOJA ZA MSINGI ZINAZOBISHANIWA.
(a)ODINGA : Hawa wanasema walishinda uchaguzi matokeo yakabadilishwa.
UHURU: Hawa wanasema matokeo yaliyotolewa yalikuwa halisi.
(b)ODINGA: Hawa wanasema mapungufu yaliyojitokeza yanatosha kubatilisha. uchaguzi.
UHURU:
Hawa wanasema ili mapungufu yabatilishe uchaguzi ni lazima mapungufu
hayo yawe yameathiri moja kwa moja namba/idadi ya kura.
(c) ODINGA: Hawa wanasema server ya tume huru ikaguliwe kwa kuwa ilitumika kubadili matokeo.
UHURU:
Hawa wanasema haiwezi kukaguliwa kwa kuwa ina code za siri ambazo
zikijulikana zitaathiri chaguzi zijazo na usalama wa taifa.
(d)ODINGA
: Hawa wanasema fomu nyingi za kukusanyia matokeo 34a, 34b na 34c
hazikutumwa kwa njia ya umeme kama inavyotakiwa na hivyo kuwa batili.
UHURU :
Hawa wanasema sheria inasema njia ya umeme ikishindwa itumike manual
hivyo baadhi ya maeneo njia hii ilifail na ikatumika manual.
(e)ODINGA
: Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe ni Kulinganisha
kinachowezekana zaidi(balance of probabilities) kwakuwa hili ni shauri
la madai kama madai mengine.
UHURU: Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe "Pasi na Shaka" (beyond reasonable doubt).
(f) ODINGA: Hawa wanasema kuna matokeo yalianza kuingia sa 11 hata kabla vituo havijafungwa.
UHURU:
Hawa wanasema kuna vituo vilikuwa na wapiga kura 20 au 50 hivyo wapiga
kura waliisha, wakafunga mapema wakahesabu na kutuma.
(g) ODINGA: Hawa wanasema baadhi ya fomu hazikusainiwa na kuwa na mihuri ya wasimamizi.
UHURU: Hawa wanasema uzembe wa wasimamizi hauwezi kufuta matakwa ya mpiga kura aliyesimama juani siku nzima.
(h) ODINGA:Hawa wanasema mwenyekiti alimtangaza mshindi hata kabla ya fomu zote kufika kutoka mashinani.
UHURU: Hawa wanasema aliona hata akizisubiri haziwezi tena kubadili matokeo.
nk, nk, nk.
5. HUKUMU.
Hukumu
itabeba jambo moja kati ya mawili. Ni kukubali ushindi wa Uhuru au
kuubatilisha. Ikiubatilisha haitasema sasa Raila ndiye rais bali
itaamrisha uchaguzi wa rais kurudiwa.
Katiba inasema uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 60 tokea siku ya hukumu.
6. ATHARI ZA HUKUMU.
Hukumu itaathiri kesi zote za uchaguzi wa wabunge , seneta nk. zilizofunguliwa nchi nzima.
Kanuni zitakazochorwa na mahakama hiyo(jurisprudence) ndizo zitazotumika katika mahakama zote za chini kutoa maamuzi yake.
Kwahiyo ni hukumu yenye athari kubwa sana na inayosubiriwa kwa hamu na gamu.
NI kesho ijumaa tusubiri tuone.
+255784482959.


Post a Comment