Meneja
wa Tawi la Samora la Benki ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc),
Leticia Ndongole, (kushoto), akimkabidhi IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka
Waning’ombe mkoani Njombe, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa
promosheni ya “Weka akiba na ushinde” inayoendeshwa na benki hiyo.Hafla
hiyo imefanyika leo Julai 18, 2017 kwenye tawi lam benki hiyo Mtaa wa
Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wengine ni washindi kutoka
kulia, ni Bw. Benester Lazaro na Bi. Grace Machemba wote kutoka Dar es
Salaam.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WATEJA
wanne wa Mwalimu Commercial Bank PLC wamejishindia zawadi za IPAD na
vocha za manunuzi baada ya kuibuka washindi kwenye Droo iliyochezeshwa
na benki hiyo kufuatia kweney promosheni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa
Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai
18, 2017 wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu wa Kitengo cha
Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (pichani juu),
alisema, Droo hiyo ilikuwa wazi kwa wateja wote waliopo na
watakaojiunga na benki kwa kufungua akaunti kwa kuweka akiba ya Shilingi
50, 000 au zaidi.
Akifafanua
zaidi Bw. Lutenganya alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2017 na
wamepokea wateja wengi ambao walishiriki kwenye Droo hiyo
iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha,
(Gaming Board of Tanzania).
Aliwaja
washindi hao kuwa ni pamoja na Bw. Shukuru Sanga, kutoka Waning’ombe
mkoani Njombe ambaye alijinyakulia IPAD, wakati Bw. Benester Lazaro, na
Grace Machemba kutoka Dar es Salaam, walijinyakulia vocha za manunuzi
kama ilivyo kwa Bi. Joyce Sangusangu kutoka mkoani Dodoma.
Akifafanua
zaidi jinsi kampeni hiyo ilivyoendeshwa, Bw. Lutenganya alisema, kadiri
mteja alipoweka akiba zaidi ndivyo alivyojiwekea nafasi nzuri ya
kushinda zawadi na amewataka wateja na wananchi wengine kuweka akiba
kwani droo nyingine itachezeshwa baadaye mwezi huu.
Aidha
alisema hudma za benki hiyo, ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki
za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali
na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kuja kufungua
Akaunti na kuweka akiba.
Alisema,
“Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, nakuwahakikishia wateja na
wananchi kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani benki inatoa
huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu ikiwemo huduma ya ATM kwenye
mtandao mpana wa UMOJA switch wenye ATM zaidi ya 200 kote nchini.
“Lakini
si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile
Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na
kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti
zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki
yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
Bw. Lutenganya akiwa na maafisa wa benki hiyo wakati akizungumzia zawadi hizo
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.
Wafanyakazi wa MCB wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshindi
wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea
kwa niabaya washindi wenzake. Kushoto ni Afisa Mikopo wa benki hiyo,
Bw.Isaya Hagamu.
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara na Masoko, cha benki ya Walimu Tanzania,
(Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB), Valence Lutenganya, (kulia),
akizungumza mbele ya washindi wa promosheni ya kwanza ya “weka akiba na
ushinde” kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es
Salaam, Julai 18, 2018. Wateja wane wa benki hiyo walijishindia IPAD na
Vocha za manunuzi, baada ya kuingia kwenye droo iliyowaibua kuwa
washindi. Kwa mujibu wa Lutenganya, mshindi ni lazima aweke akiba si
chini ya shilingi elfu 50,000 au kufungua alkaunti na kuweka kiasi hicho
cha akiba na hivyo kuingia kwenye promosheni hiyo moja kwa moja. Kutoka
kushoto ni Meenja wa tawi la benii hiyo, Leticia Ndongole, Mshidni wa
IPAD, Shukuru Sanga, Grace Machemba, (Voucher), and Benester Lazaro,
also he won a voucher.
Afisa
Mikopo wa MB, Bw. Isaya Hagamu, (kushoto), akimkabidhi zawadi ya vocha
ya manunuzi, mshindi wa promosheni ya "Weka akiba na ushinde"
inayoendeshwa na benki hiyo, Bw. Benester Lazaro wa jijini Dar es Salaam
hukuMeneja wa tawi la Samora la benki hiyo, Bi. Leticia Ndongole,
akishuhudia.
Bw. Lutenganya(kulia). akimpongeza Bw. Lazaro kwa ushindi. Kushoto ni Bi Leticia Ndongole
Bi Leticia Ndongole(kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPD, Bw. Sanga.
Meneja
wa Tawi la Benki wa Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia
Ndongole, (katkati), akishuhudia jinci Meneaj wa Huduma kwa wateja wa
tawi hilo, Flora C. Mbogo, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi
mteja wa benki hiyo, Grace Machemba, baada ya kuwa mionhoni mwa washindi
wa promosheni ya weka akiba na ushinde ya benki hiyo. Hafla ya
kukabidhi zawadi hizo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mtaa wa
Samora jijini Dar es Salaam Julai 18, 2017. Ambapo washindi wengine
waliibuka na IPAD na vocha.
Mwanahabari akiwa kazini akitekeleza majukumu yake wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment