Pages

June 24, 2017

KIJIJI CHA SHUJAAZ CHAFUNGULIWA KATIKA MASHINDANO YA EAC 2017 MJINI MOSHI

Mwakilishi wa Taasisi ya Wel tel Story watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz,Alan Lucky akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kufunguliwa kwa kijiji cha Shujaaz katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki maarufu kama East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika shule ya Sekondari Moshi Ufundi .
Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo mbalimbali hasa ya Kilimo .
Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma ,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo.
Mjasiliamali Khalfa Muslim akitoa elimu jinsi ya kutengeneza mchanganiko wa Matunda kwa vijana waliotembelea kijiji cha Shujaaz kilichopo katka viwanja vya Shule ya sekondari Moshi Ufundi yanapofanyika mashindano ya East Africa Cup 2017.
Mjasiliamali Holo Bukombe akionesha bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka katika vifungashio maalumu na kuongeza thamani ya bidhaa husika.
Afisa Masoko wa kamuni ya YARA Ltd ,Linda Byaba akitoa elimu kuhusu kilimo bora na chenye tija na jinsi ya kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya Mbolea kwa Mwakilishi wa taasisi ya Wel tel Story ,Alan Lucky.
Muonekano wa kijiji cha Shujaaz kilichopo katika Shule ya Sekondari Moshi Ufundi ambako elimu mbalimbali hususani za Kilimo pamoja na michez kwa vijana imekuwa ikitolewa.
Baadhi ya watoto wakishindana michezo mbalimbali (Games) katika kijiji cha Shujaaz.
Vijana wengine wamepaa fursa ya kucheza mchezo wa mitupo ndani ya kijiji hicho.
Vijana wengine walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hasa vya kuimba na kucheza na kuambulia zawadi kutoka Shujaaz.

Na Dixon Busagaga wa Glob ya Jami ,Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...