TUMEZOEA
kuwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana
“mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Ila sahihi ni “mtindio
ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi
ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi, mwili
mfupi, utofauti wa tambo la kichwa, vidole vya mikono na miguu, nk.
Mbali na kuwanyanyapaa, jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa
kuendeleza wenye ulemavu. Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika,
mwenye “Mtindio Ubongo “ (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa
wa upigaji picha. Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro
akaeleza: “Wametoka vijana wengi kwenye nchi zilizoendelea, wengine
wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu
mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo
bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku, picha yake
imeshinda...” Mwasisi wa kujitolea wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl
of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite na wazazi wake Samwel,
Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi Migiro na
kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula ,
pia alikuwepo.
Afisa
Utawala Ubalozini, Rose Kitandula na Mheshimiwa Balozi wakiwa na Samwel
Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina
Haika Petitt.
Picha
ya pamoja . Toka kushoto, Mjomba wake Sam, Hassan Mshangama, Mama Sam,
Sophie Mshangama, Mony Teri Pettite, Penina Haika Pettite, Balozi
Migiro, Sam Mwanyika, Rosa Kitandula (Afisa Utawala Ubalozini), na
Philip Mwanyika (baba wa mshindi)
Balozi
Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa “Pearl of People
with DownSyndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye
Mtindio Ubongo (Down Syndrome).
Tuzo ya Stephen Thomas
No comments:
Post a Comment