Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano
wa mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya
umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana.
Katibu
Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo,akifungua mkutano wa
mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma
katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mwenyekiti wa Sekta ya Uwazi na Uwajibikaji katika Ujenzi (Cost
Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili na Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa
la Ujenzi,Elias Kissamo. (PICHA NA ELISA SHUNDA)
Wadau wa masuala ya ujenzi wakifuatilia kwa umakini wakati mkutano huo ukiendelea.
Imeandaliwa na Mtandao
Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili,akizungumza katika mkutano huo.
Katibu
Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo akiwa kwenye picha ya
pamoja na viongozi wa Baraza la Taifa la Ujenzi Tanzania na wadau wa
masuala ya ujenzi nchini.
Imeandaliwa na Mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com mawasiliano elisashunda@gmail.com namba ya simu 0719976633.
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI itaokoa angalau Sh.bilioni 900 kwa mwaka endapo itafanikiwa katika utekelezaji wa Mkakati Uwazi katika Ujenzi (CoST).
Aidha kupitia mkakati huo, miradi mbalimbali ya mashirika ya umma 10
inatarajiwa kufanyiwa tathmini itakayokamilika ifikapo Julai mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano wa mashauriano ya utoaji wa taarifa za miradi
ya ujenzi wa miundombinu ya umma wa baraza la wajenzi, Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais Ikulu, Peter Ilomo alisema kuwa mkakati huo utapunguza
rushwa na upotevu wa fedha za Serikali.
Ilomo alisema CoST itaisaidia Serikali na umma kujua fedha zinavyotumika
katika ujenzi wa miundombinu, kuokoa fedha za umma kwa kupunguza rushwa
na kuboresha usimamiaji wa utekelezaji wa miundombinu.
Mwenyekiti wa CoST, Kazungu Magili alitaja mashirika yatakayofanyiwa
tathmini na kuweka wazi miradi yake kuwa ni, Wakala wa Majengo (TBA),
Wakala wa Barabara (Tanroads) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)/.
Mashirika mengine ni mifuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii ya NSSF, GEPF,
LAPF, Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee
na Watoto na kutoa taarifa kwa umma ambapo utaweza kuitumia kufuatilia
utekelezaji wa miradi husika.
Alisema kupitia tathmini hiyo, CoST itapata fursa ya kutambua majengo
yaliyojengwa kwa mujibu wa vigezo ama chini ya kiwango halisi cha fedha
zilizotolewa na thamani ya jengo husika.
Magili alisema ikitokea kuna baadhi ya miradi imejengwa chini ya kiwango
itafikishwa katika mamlaka mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) na
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili hatua mbalimbali
zichukuliwe.
Aidha alisema kuwa awali kabla ya kuanzishwa mkakati huo mambo mengi
yalikuwa hayawekwi wazi hali ambayo imekuwa ikisababisha upotevu wa
fedha.

إرسال تعليق