MKUU WA MKOA WA ARUSHA,MRISHO GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDISHI WA HABARI




Mkuu wa wilaya ya Arusha , Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo la kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa  pamoja na wadau mbalimbali.

Mwenyekiti wa Arusha press club (APC),Claud Gwandu akizungumza na katika kongamano hilo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo akiwa kwenye kongamano hilo.
Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Mussa Juma (kushoto) na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha Channel Ten, Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV, Anold Rweyemamu.Picha na Vero Ignatus BlogMkurugenzi wa jiji la Arusha,Athuman Kihamia(kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha,Dk Wilfred Soileli


Na.Vero Ignatus, Arusha.


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamano la  kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa lililowashirikisha wadau wa habari katika kuangalia  pamoja na  mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.

Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita  na kuangalia mambo gani serikali inayapa kipaumbele na kuzitafutia ufumbuzi  changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa  ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

“Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .

Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.

Post a Comment

أحدث أقدم