
Zifuatazo
ni Taarifa za Mechi za Vinara Chelsea walipocheza na Stoke City huko
Stamford Bridge na nyingine huko Old Trafford kati ya Manchester United
na Middlesbrough ambao ni maarufu kama Boro.
CHELSEA 4 STOKE CITY 2
Vinara wa Ligi Chelsea wamekwenda Pointi 9 mbele baada ya kuichapa Stoke
City 4-2 na kuifikia Rekodi ya Arsenal ya kushinda Mechi 13 mfululizo
za Ligi hii waliyoiweka Msimu wa 2001/02.
Bao za Chelsea hii Leo zilifungwa na Cahill, Dakika ya 34, Willian, 57 na 65, na la Diego Costa la Dakika ya 85.
Bao za Stoke zilipigwa Dakika za 46 na 64 kupitia Martins Indi na Peter Crouch.
MANCHESTER UNITED 2 MIDDLESBROUGH 1
LICHA ya maamuzi mabovu ya Refa Lee Mason ikiwemo kuwanyima Bao safi la
Zlatan Ibrahimovic, Manchester United walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na
kusawazisha Dakika ya 85 na Dakika moja baadae kupiga Bao la ushindi
katika Mechi waliyoitawala kabisa.

Kipindi
cha Kwanza, Man United walifunga Bao safi kupitia Ibrahimovic na Refa
Mason kulikataa na Gemu kubakia 0-0 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 67, bila kutegemewa, Boro walitangulia
kufunga kwa Bao la Grant Leadbitter na kuelekea kumpa Msaidizi wa zamani
wa Jose Mourinho, Aitor Karanka, ambae ni Meneja wa Middlesbrough,
ushindi huku Kipa wa zamani wa Man United Victor Valdes akiwa nguzo yao
imara akiwanyima Man United bao kadhaa za wazi.

Lakini
Dakika ya 85, kazi njema ya Ibrahimovic ilimpa mwanya Anthony Martial
kusawazisha na Dakika 1 baadae Krosi ya Juan Mata, alieingizwa Kipindi
cha Pili, kuunganishwa kwa Kichwa na Paul Pogba na kuwapa ushindi Man
United wa 2-1 wakikumbusha enzi za Sir Alex Ferguson za ushindi murua wa
Dakika za mwisho hasa Leo ikiwa ni Siku ya Kuzaliwa ya Lejendari
alietimiza Miaka 75 akiwepo pia Uwanjani hapo Old Trafford kushuhudia
Mechi hii.
MOURINHO AKIONGELEA KWANINI BAO LA IBRAHIMOVIC LIMEKATALIWA:
“Refa Bwana Mason ndie anaejua lakini anajua alifanya kosa. Nadhani
inasikitisha kwa sababu Marefa wanasikitika wakifanya makosa!”

VIKOSI: Manchester
United (4-3-3): De Gea, Valencia, Bailly, Smalling (Rashford 72), Blind
(Rojo 64), Herrera, Fellaini (Mata 64), Pogba, Mkhitaryan, Ibrahimovic,
Martial.
Subs not used: Romero, Jones, Lingard, Schweinsteiger
Goals: Martial 85, Pogba 86
Booked: Blind
Middlesbrough (4-5-1): Valdes, Chambers, Bernardo, Gibson, Friend,
Traore(Fabio 82), Leadbitter(Clayton 78), Forshaw, De Roon,
Downing(Ramirez 64) Negredo.
Subs not used: Guzan, Ayala, Rhodes, Stuani.
Goal: Leadbitter 67
Booked: Chambers
Referee: Lee Mason 5.5

إرسال تعليق