Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua
rasmi daraja hilo la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja
Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi
za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa
Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa
Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi
wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi
wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Ujenzi
wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani
Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya
Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo
la JICA. Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha
TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa
kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi
wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera –
Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka.
Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la
Rusumo mara baada ya uzinduzi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja
na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio
hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi
zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na
Kimataifa.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo








Post a Comment