Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi (Mb), akitoa maagizo kadhaa wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo; Prof. Wilbard Kombe na kulia kwake ni Mwenyekiti mstaafu, John Lubuva.
Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji; Prof. Wilbard Kombe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti
mstaafu wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji; Bwn.John Lubuva akitoa
taarifa fupi ya bodi hiyo, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya katika ukumbi
wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) ametangaza
rasmi mwisho wa kutumia Makampuni ya nje katika kazi za kuandaa Master
plan. Mhe. Lukuvi aliyasema hayo wakati akizindua rasmi bodi ya wataalam
wa Mipango Miji Wizarani hapo.
Lukuvi
amesema nchini kuna wataalam wengi na wenye elimu ya kutosha kwa ajili
ya kufanya kazi ya kuandaa Master plan, lakini kumekuwa na taratibu za
kutafuta wataalam hao kutoka nchi za nje. Alisema; “ Ninaagiza kuwa sasa
ni mwisho wa kuajiri makampuni ya nje, kazi za master plan zisimamiwe
na bodi hii kwa kutumia makampuni ya humu humu nchini”.
Ameendelea
kusema kuwa’ “ Sasa Bodi ya Wataalam wa Mipango Miji itapaswa kuhusika
kikamilifu katika zoezi la Upangaji, upimaji na umilikishwaji wa ardhi
kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuhakikisha kuwa suala la uwazi
katika upangaji miji linazingatiwa”.
Vile
vile alisema kuwa bodi itapaswa kuhakikisha Wananchi wanashirikishwa
kikamilifu katika kulipia gharama kadhaa kwa huduma wanazopatiwa na
bodi. Mhe. Lukuvi alisema kuwa bodi hiyo haitaitwa tena bodi ya Mipango
Miji, bali itajulikana kama bodi ya Mipango Miji na Vijiji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti mpya wa bodi; Prof. Wilbard Kombe alimuomba
Lukuvi kuzitaka Halmashauri kushiriki vyema katika kutoa elimu kwa umma
kwa kuwa na utayari wa kutoa taarifa zinazopaswa kuwasilishwa kwa
Wananchi kwa wakati ili waweze kuelewa vyema kuhusu mipango inayohusu
maeneo yao.

Post a Comment