Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi
matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari
wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika
uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa
hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi
wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao
katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi
lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa
pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini
Malaysia.
Kobe
wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na
Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori
wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada
wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. (Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)
No comments:
Post a Comment