Ndege ya shirika moja la ndege la Urusi, iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200, imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri.Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi.Vyombo
vya habari nchini Misri vinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana na
magari ya uokozi zaidi ya 20 zimetumwa katika eneo la ajali.Rais
wa Urusi Vladimir Putin ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa
za waathirika na kuagiza uchunguzi ufanyike, huku akitangaza kesho kuwa
ni siku ya maombolezo.
No comments:
Post a Comment