Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo October 31 kwa wekundu wa Msimbazi Simba kuwakaribisha Maji Maji FC wanalizombe kutokea Ruvuma Songea. Simba ambayo bado inatajwa kuwa hakuna mahusiano mazuri baina ya kocha Dylan Kerr na uongozi ambao inadaiwa wanaamini kuwa timu haipo katika kiwango kizuri.
Hata hivyo Simba
waliingia uwanjani wakiwa na morali ya kutaka kupata ushindi kwani
walifanikiwa kupata ushindi wa jumla ya goli 6-1, lakini kitu cha
kuvutia ni pale ambapo wachezaji wa Simba walikuwa
wakifunga na kwenda kushangilia na kocha wao kila goli, kitendo ambacho
kilitafsiriwa kama kuonesha kuendelea kumkubali aendelee kuwepo katika
timu.
Magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib aliyefunga hat-trick kwa kuanza kufunga goli la kwanza dakika ya 8, 14 na 42 akakamilisha idadi ya goli zake tatu, Hamisi Kiiza alifunga goli mbili katika mchezo huo dakika ya 32 na dakika ya 81 baada ya dakika ya 71 Hussein Mohamed ‘Tshabalala’ kufunga goli la tano kwa Simba, Maji Maji FC walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Ditram Nchimbi.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 31
- Kagera 0 – 2 Yanga
- Coastal Union 1 – 1 Mbeya City
- Mtibwa Sugar 4 – 1 Mwadui FC
No comments:
Post a Comment