Mwenyekiti
wa National Governance Internet Forum ambaye pia ni Rais wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akiwakaribisha
wadau wa mitandao na watumiaji wa intaneti kwenye jukwaa hilo kabla ya
kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kufungua rasmi jukwaa
hilo.. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research
Network (TERNET), Amos Nungu na Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard. (Picha
zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi Mwetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO),
limewaomba wadau wa habari hasa wa matumizi ya intaneti kuzingatia
maadili na usiri katika kazi zao ili kutovunja sheria zilizowekwa na
mamlaka husika likiwemo suala la sheria ya mtandao iliyopitishwa hivi
karibuni nchini Tanzania.
Hayo
yameelezwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin
Yusuph aliyekuwa akimwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues
katika Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF),
lililofanyika mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
UNESCO
inaamini masuala ya usiri katika mitandao ni njia bora zaidi za
kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili na usio zingatia taaluma.
Ambapo
amebainisha kuwa, takribani Asilimia 84 ya Mataifa duniani wamegundua
hawana sheria madhubuti ya kulinda uhuru wa usiri kwa wananchi kupitia
mitandao hivyo ni muhimu kuzingatia taaluma na maadili kwenye matumizi
ya intaneti hasa kwa kipindi hichi.
“UNESCO
inaamini mambo muhimu ya kuzingatia juu ya matumizi ya mitandao ikiwemo
kuwa na Uwazi, Upatikanaji na Ushirikishi. Kwa hayo machache, mjadala
huu wa matumizi ya mtandao unaweza kufanikiwa na sie tunapenda kuungana
na nyinyi katika kushirikiana katika suala hili” alieleza Ofisa Miradi
ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday
Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya
mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari
Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano
COSTECH jijini Dar. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na
Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Al Amin Yusuph aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO na kulia
Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum, Kenneth Simbaya.
Aidha,
katika mkutano huo, imeelezwa kuwa, matumizi makubwa ya mtandao wa
kompyuta (intaneti) yatasaidia ongezeko la pato la taifa (GDP).
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya jukwaa la
mtandao wa intaneti (IGF) Kenneth Simbaya wakati wa jukwaa hilo ambapo
amebainisha kuwa, katika matumizi yake ni muhimu sana kujadili
kutengeneza kesho wanayoitaka watanzania katika matumizi ya mtandao.
Ameeleza
chombo cha IGF kimelenga kuangalia maendeleo ya mtandao nchini usalama
wake na matumizi ya mtandao yanayoelenga kubadilisha maisha ya
watanzania kwani chombo hicho nchini Tanzania kimeundwa kutokana na
mkutano wa kimataifa wa jamii ya wanahabari (WSIS) waliotaka kuwepo na
jukwaa kuangalia matumizi ya matandao kutokana na kuongeza kwa haja ya
matumizi.
Simbaya
amesema Majukwaa hayo yanatakiwa kuzungumza kuhusu sera kwa lengo la
kuangalia uendelevu wake , usalama, ukuaji wa mtandao wenyewe na
menejimenti yake.
Kwa
upande wake Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akithibitisha
umuhimu wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo, alielza kwamba kama
kutakuwepo na ongezeko la watumiaji angalau kwa asilimia 10 pato la
taifa litaongezeka kwa asilimia 1.4. zaidi.
Ambapo
anaendelea kubainisha kuwa, kwa sasa idadi ya watumiaji wa mtandao
wameongezeka kufikia asilimia 11 na kwamba lugha ya mtandao kwa sasa
inaathiri watu mbalimbali kwa namna njema na namna mbaya.
Jukwaa
hilo pamoja na kuzungumza kuhusu uendelevu wake pia ulizungumzia
sheria , kanuni na taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa katika matumizi na
utawala wa intaneti ili kuzifanya zitumike kwa makusudio mema zaidi.
Naye
mtaalamu wa masuala ya mtandao wa intaneti, Maxence Melo kutoka Jamii
Forum amesema kwamba mpaka sasa anaona kwamba matumizi ya mtandao
Tanzania bado salama ingawa juhudi lazima ziendelee kufanyika
kuhakikisha kwamba hali ya usalama inaendelea kuwapo.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph
aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO akitoa salamu za shirika la UNESCO
wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya
mtandao (NIGF) ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari
Tanzania (UTPC).
Katibu
Mtendaji wa Tanzania Education and Research Network (TERNET), Amos
Nungu akitoa salamu za TERNET kwa wadau waliohudhuria jukwaa hilo.
Mtaalamu
kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akiwasilisha mada iliyoelezea umuhimu
wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo wakati wa jukwaa hilo.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki waliohudhuria jukwaa hilo
wakifuatilia "presentation" iliyokuwa ikitolewa na Mtaalamu kutoka TCRA
Dk. Emmanuel Manasseh (hayupo pichani).
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph kwa mtaalamu
kutoka TCRA (hayupo pichani) kama wana mipango gani kuhakikisha kuwa
kutakuwepo na masafa ya kutosha kwa miaka mingi ijayo kwaajili ya
wananchi wa vijijini na wale wasio na uwezo.
Picha ya pamoja.
Maxence
Melo kutoka Jamii Forum akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
jukwaa lililowakutanisha kwa pamoja wadau wa masuala ya mitandao ya
intaneti.
Maxence
Melo kutoka Jamii Forum (katikati) akipata picha ya pamoja na wajumbe
wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Fredy Njeje wa Blog za Mikoa (kulia)
na Mr. Verbs.
No comments:
Post a Comment