Ni taarifa ambazo zimechukua headlines usiku wa July 12 baada ya watu wanaosadikiwa kuvamia kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga Dar na kuuwa watu saba.
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi (IGP),
Ernest Mangu…’Nasikitika kuwapa taarifa kuwa majambazi walivamia kituo
cha polisi cha Stakishari na kupiga risasi na kuua Askari polisi wanne
na raia watatu. Majambazi hao walikuja kama raia wakawaida wanaohitaji
huduma walipofika kituoni na kuulizwa shida yao nini ndipo walipoanza
kuwashambulia askari walio kuwa kituoni’ – Ernest
‘Raia waliouwawa ni raia ambao walikuwa
wamekuja kituoni kutoa taarifa za matukio ya kwao ya kawaida wapo pia
askari ambao wamejeruhiwa na raia waliojeruhiwa wapo hospitali wanapata
matibabu’ – Ernest Mangu
‘Nikweli kuna silaha ambazo zimeporwa
miongoni ni zile ambazo za askari ambao walikuwa ulinzi hapa na zingine
zilikuwa chumba cha mashitaka.uchunguzi unaendelea kujua silaha ngapi
zimeporwa wakati tukipata taarifa mpya tutazitoa’ – Ernest Mangu
‘Tukio hilo la kusikitisha lazima sheria
ichukue mkondo wake kuwapata hao waliohusika na tukio hilo.kama
mnakumbuka tukio kama hili lilitokea Ushirombo walivamia kituo kama hiki
walisababisha mauaji kwa Askari sisi hatutachoka tutahakikisha
tunapambana nao mpaka tunawapata’ – Ernest Mangu
No comments:
Post a Comment