Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki
zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya
Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana
na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Mkurugenzi
wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi
kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi
wa Manispaa ya Ilala wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari
ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya
Mazingira. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Wadau mbalimbali kutoka Green
WastePro Ltd, Manispaa ya Ilala, Forum CC pamoja na wasanii mbalimbali
wakiendelea kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi kata ya
Kivukoni katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Hali ilivyokuwa kabla ya kufanya usafi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi
wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shay o(kulia) wakati wa zoezi
la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa
ni wiki ya Mazingira. Kushoto ni Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi, Lukac Mhavile "Joti"
Wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green
Waste Pro Ltd wakiendelea zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya
Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akizungumza jambo na Afisa
Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda wakati wa zoezi la kufanya
usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi eno la Aga Khan jijini Dar ikiwa
ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Mkurugenzi
wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo ( wa tatu kutoka kulia)
akifaya usafi na wadau mbalimbali kwenye wiki ya Mazingira eneo la Agha
Khan jijini Dar, wa pili kutoka kulia ni Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena.
Afisa
Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda akizungumza jambo baada
ya kumalizika kwa zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya Hindi.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) ili kuzungumza na wadau
mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya
Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira, wa kwanza
kulia ni Afisa Usafishaji Manispaa ya Ilala, Bw. Charles Wambura.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akisitiza jambo kwa wadau
walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga
Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu
wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea
katika manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd.
No comments:
Post a Comment