Miongoni
mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni
Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata
kupitia Radio One pia.Charles
Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha
Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon
Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
Naibu
Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alithibitisha Hillary kutarajiwa
kujiunga na Azam Media akiwa na historia nzuri kwenye vyombo vya habari
kuanzia alipoanza mwaka 1994 Radio one na kabla ya hapo alitokea radio
Deutsch Welle na mwaka 2006 alijiunga na BBC.


إرسال تعليق