Arusha.Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing,amesema serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu kama njia mojawapo ya kupiga vita umasikini.
Alisema hayo jijini
Arusha wakati akikabidhi madarasa mawili katika Shule mpya ya Msingi ya Muriet
iliyopo Kata ya Sokon 1 yaliyojengwa kwa msaada na kampuni ya ujenzi ya Jiangxi
Geo-Egineering(Group)Corporation.
“Uwepo wa Shule hii ni
ukombozi mkubwa kwa watoto hawa ambao hawalazimiki
kutembea umbali mrefu kwaajili ya kutafuta elimu ambayo ni msingi wa maendeleo
ya kila mtu na nyenzo ya kupambana na umasikini,”alisema Dk Lu
Hata hivyo aliishauri
serikali kuongeza walimu idadi ya walimu kutoka wanane waliopo ukilinganisha na
idadi ya wanafunzi 350 walioandikishwa darasa la kwanza mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya
Arusha,Christopher Kangoye alisema kampuni hiyo imeonesha uungwana wa kuchangia
miradi ya maendeleo baada ya kuona mahitaji wakati ikijenga miundombinu ya jiji
na kuliweka Jalala Kuu katika hali ya kisasa ambayo haithiri afya za wananchi
wanaozunguka eneo hilo.
“Ningependa makampuni mengine
yaige mfano ulioneshwa na Jiangxi Geo-Engineering kwa kutoa sehemu ya faida
waliyoipata kuirejesha kwa jamii ili inufaike na kama jamii zingine,elimu ni msingi wa maendeleo yetu,”alisema Kangoye
Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa kampuni hiyo,Ye Chengbiao alisema
wametumia kiasi cha Sh 25 milioni kukamilisha ujenzi huo na kuweka meza na viti
vya kisasa baada ya kupata ushirikiano wa serikali ya halmashauri ya Jiji na
wananchi wa Muriet.



إرسال تعليق