Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)linasikitika kutangaza kifo cha
Brigedia Jenerali Richard Mwilipanga Lupembe (mstaafu) kilichotokea
tarehe 30 Machi 2015, Brigedia
Jenerali Lupembe (mstaafu) alizaliwa mwaka 1945 katika Wilaya ya
Njombe, Mkoa wa Njombe, Kijiji chaUtengule, Kata ya Lupembe, Tarafa ya
Lupembe. Alisoma
shule ya Msingi Malangali, Shule ya Sekondari Malangali na shule ya
Sekondari H.H. Agakhan na kuhitimu Kidato cha Sita mwaka 1964. BrigediaJenerali
Lupembe alijiunga na Jeshi tarehe 26 Agosti, 1964 na Kutunukiwa
kamisheni tarehe 28 Julai, 1966. Alistaafu utumishi Jeshini kwa umri
tarehe 30 Juni, 1998.
Katika
utumishi wake alishika madaraka mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa
Utendaji Kivita Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa mafunzo, na Mwambata
Jeshi, Msumbiji, 1993hadi alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 30 Juni
1998.
Marehemu ameacha mke na watoto.
Mwili wa
marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 04 Aprili, 2015 kuanzia saa
3:00 hadi 4:00 asubuhi katika eneo maalumu la hospitali kuu ya Jeshi
Lugalo na baadaye kupelekwa nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kuagwa
kifamilia kisha mazishi rasmi kufanyika saa 9:00 Alasiri katika makaburi
ya Kinondoni.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI RICHARD MWILIPANGA LUPEMBE (MSTAAFU) AMINA
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na MahusianoMakao Makuu ya Jeshi, Upanga


إرسال تعليق