Mussa Juma, Arusha.
MFUKO wa Maendeleo ya jamii(TASAF) umezindua mradi wa kupunguza
umasikini kwa watu milioni 3.1 kutoka halmashauri 14 za mikoa ya Arusha
na Njombe unaogharimu kiasi cha dola 16.4 milioni ambazo ni zaidi ya Tsh
30 bilioni.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akizindua mradi
huo ambao ni sehemu ya mradi wa tatu wa kupunguza umasikini nchini,
alisema wananchi 3.1 milioni watanufaika katika kupata maji safi,huduma
bora za afya na elimu.
“katika awamu hii, TASAF inalenga kuondoa mapungufu katika huduma muhimu
za kijamii,ikiwepo kusaidia jamii kutekeleza miradi ya umwagiliaji na
shughuli za kuongeza kipato”alisema
Ntibenda alizitaja halmashauri
ambazo zipo katika mradi huo kuwa ni Jiji la Arusha,halmashauri ya
Monduli,Ngorongoro, Longido,Meru na halmashauri ya Karatu.
Alisema
kwa mkoa wa Njombe, halmashauri ambazo zitagushwa ni
Ludewa,Makete,Njombe,halmashauri Wanging’ombe,halmashauri za miji ya
makambako na halmashauri ya Njombe.
Awali,Mkurugenzi mkuu wa TASAF , Ladislaus Mwamanga alisema fedha za
kutekeleza miradi hiyo, zimetolewa na umoja wa nchi za wazalishaji wa
mafuta (OPEC) ambapo awamu kwanza Ililenga mikoa ya Mtwara na Lindi
ambapo kiasi cha dola milioni 10 zilitumika.
Alisema awamu pili ya mradi huo, pia ilitumika mikoa ya Mtwara na lindi
ambapo kiasi cha Dola milioni 12 zilitumika na kuweza kuwa na mafanikio
makubwa kutokana na kufanikisha miradi kadhaa ya maendeleo na kuchochea
maendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasai
alieleza kuridhishwa na TASAF kuichaguwa halmashauri ya Karatu kuwa ni
miongoni mwa halmashauri 14 ambazo zitanufaika na mradi wa TASAF awamu
ya tatu.
Lazaro alisema anauhakika halmashauri yake na halmashauri
nyingine zilizopata mradi huu, zitaweza kuchangia kuondoa matatizo mbali
mbali ya kijamii na hivyo kuinua hali za maisha ya wananchi ili lengo
la TASAF lifikiwe.
CREDIT: SAUTI YA MNYONGE
No comments:
Post a Comment