
Mbunge
wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa
Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao
wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.”
Akizungumza
na gazeti hili jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la
Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli
aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu ya
polisi.
Lema
alisema maafisa hao, ambao walikuwa wanatumia gari dogo, baada ya kufika
hotelini hapo, waliomba aitwe na aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi
makao makuu ya polisi kwa mahojiano.
“Niliwauliza
nikaandeke maelezo juu ya nini, walijibu kifupi wao ni chombo cha dola na
walisema wametumwa na viongozi wa juu wa polisi na hawakuwa tayari kutaja
tuhuma zangu,” alisema Lema.
Alisema
baada ya polisi hao kusisitiza kutaka kumchukua, aliwaomba aende chumbani
kujiandaa kabla ya kuwasiliana na viongozi wa chama chake na familia yake.
“Niliposhuka
chini sikuwakuta na ndipo nikashauriana na viongozi wa chama hicho na kuamua
kuondoka jana mchana Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
Hata hivyo, alisema Chadema leo wanatarajia kutoa tamko juu ya kauli ya
Rais Jakaya Kikwete kuwataka wanachama wa CCM kuondoa unyonge dhidi ya
wapinzani hasa pale wanapodaiwa kupigwa

Post a Comment