Filbert Rweyemamu,Arusha
Taasisi ya Gola Foundation Ltd na wafanyabishara wa
jiji la Arusha wameunda kamati maalumu
ya kuwasaidia watoto wanaoishi maisha magumu itakayofanya kazi kwa kipindi cha
miaka miwili ijayo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuichangia taasisi
inayowasaidia watoto na vijana kutoka kwenye mazingira ya kuishi mitaani iliyofanyika kwenye uwanja Makumbusho ya Taifa Elimu Viumbe.
Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Bushbuck ya jijini hapa,Mustafa Panju
alisema maisha wanayoishi watoto hao kwa sasa kila mtu anapaswa kubeba lawama.
Alisema ili misaada inayotolewa iweze kuwa endelevu wameunda
tume maalumu itakoyosimamia shughuli za fedha na kuchambua kwa ukaribu nini
mahitaji ya watoto na vijana hao kwa lengo la kuwajengea misingi bora ya maisha
yao.
“Tunapaswa kushirikiana kila mmoja wetu kuhakikisha tunawasaidia
kuwaondoa kwenye mazingira wanayoishi ili wawe kama wananchi wengine na kamati
hii itaweka mikakati ya kibiashara ambayo itakua endelevu ambayo ndani ya miaka
miwili tutafanya tathmini kuona mafanikio yake,”alisema Mustafa
Mratibu wa Gola
Foundation ,Pascal Matimba alisema kupitia kikundi cha New Hope Street Kids
kinasaidia watoto na vijana 120 katika mitaa mbalimali wanaosaidiwa kutoka
mazingira hatarishi ambayo mara nyingi huwafanya kushindwa kupata elimu na
kuishia kutumia madawa ya kulenya.
Alisema vijana hao wameonesha nia ya kubadilika na wako
tayari kujishughulisha na kazi za kilimo,burudani na wengine kujiunga na vyuo
vya ufundi na shule za sekondari na msingi.
Katika risala iliyosomwa na mmoja wa watoto hao,John Laiser
alisema wameweza kupata bima ya matibabu na baadhi yao kupata udhamini wa
masomo huku wakilaumu Polisi kwa kuwanyanyasa mitaani ambako ndio makazi yao.
Mpango huo unalenga kuwasaidia vijana hao kuwafungilia
miradi ya kujiwezesha kiuchumi ,kiasi cha Sh 20 milioni kilipatikana.
Miongoni mwa wanaounda kamati hiyo ni Sailesh Pandit,Mustafa Panju,Khasim Mamboleo na Muslim Remtulah
No comments:
Post a Comment