TUME YA USHINDANI NCHINI(FCC)YAKAMATA SIMU FEKI NA VIFAA MBALIMBALI VYENYE THAMANI YA SH 200 MILIONI ARUSHA
Afisa
Mkaguzi wa Tume ya Ushindani(FCC)Michael David akizungumza na waandishi
wa habari kwenye Kituo cha Polisi jijini Arusha baada ya kufanikiwa
kukamata Simu bandia 215 za mikononi na vifaa vingine vyenye jina la
Samsung wakati sio halisi.Vifaa vitateketezwa kwenye Dampo Kuu la Muriet nje kidogo ya jiji la Arusha.
Baadhi ya Simu,Chaja na mifuniko yenye nembo ya kampuni ya Samsung vilikamatwa kwenye maduka mbalimbali jijini Arusha.
Afisa
Mkaguzi wa Tume ya Ushindani(FCC)Michael David akionesha moja ya bidhaa
bandia zilizokamatwa leo.Amewataka wananchi kununua bidhaa halisi kwa
Mawakala waliohidhinishwa ili kuepuka madhara ya kiafya.
No comments:
Post a Comment