JESHI la
Anga la Marekani limetangaza kuwa limefanyia majaribio kombora la
Balestikilinaloweza kuvuka mabara na kwamba majaribio hayo ni ujumbe kwa
walimwengu kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Anga la Marekani, kombora la
Minuteman-III lilifanyiwa majaribio mapema Jumatatu katika kituo cha
Jeshi la Anga cha Vandenberg huko California. Taarifa ya Jeshi la Anga
la Marekani imesema: Majaribio hayo ya kombola la balestiki la nyuklia
yanaonesha picha ya wazi kwa walimwengu kuhusu uwezo wa kombora ya
Minuteman-III ambalo linaweza kulenga mahala popote.
Kombora
la Balestiki linavyolipuka.Kwa kutilia maanani kwamba Jeshi la Anga la
Marekani haliwezi kutumia makombora ya Peace Keeper kwa mujibu wa
makubaliano ya silaha ya START II (Strategic Arms Reduction Treaty),
kombora la Minuteman-III litakuwa kombora pekee la balestiki linaloweza
kuvuka mabara la jeshi la Marekani. Kombora hilo linavishwa kichwa cha
silaha ya nyuklia aina ya W87 ambacho kina uwezo mkubwa wa uharibifu.
Majaribio hayo yamefanyika sambamba na mazoezi ya kijeshi yanayoendelea
kufanywa na majeshi ya shirika la NATO huko Ulaya mashariki.
Inaonekana kuwa kwa majaribio ya kombora hilo la nyuklia, jeshi la Anga la Marekani linafuatilia malengo kadhaa.
Kwanza ni
kuwa Marekani inataka kuonesha misuli na uwezo wake wa silaha za
nyuklia kwa wapinzani wake wakubwa hususan Russia. Katika kipindi cha
miaka kama miwili iliyopita jeshi la Russia limefanya majaribio mtawalia
ya makombora yanayoweza kuvuka mabara (Intercontinental Ballistic
Missile au IBM) na hata kurusha makombora kama hayo kwa kutumia
nyambizi. Kwa msingi huo Marekani ilikuwa ikinyemelea fursa ya
kukabiliana na majaribio hayo ya silaha za nyuklia ya Russia.
Suala la
pili ni kushadidi mivutano baina ya Russia na NATO huko Ulaya Mashariki
ambako kumezifanya pande hizi mbili zijizatiti kwa silaha na majeshi
katika eneo hilo na katika Bahari Nyeusi. Kwa msingi huo Marekani
inataka kumuonesha adui wake yaani Russia, kwamba iwapo mgogoro huo
utaendelea inaweza kutumia silaha zake za nyuklia.
Marekani
ni miongoni mwa wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za nyuklia duniani na
ndiyo nchi pekee ambayo hadi sasa imetumia silaha hizo kuua watu wa
taifa jingine. Nchi hiyo kinyume na ahadi zake za kupunguza maghala yake
ya silaha za nyuklia, ingali inastawisha na kupanua zaidi silaha hizo
na kuzifanyia majaribio.
Marekani
pia inasasisha na kuziboresha zaidi silaha zake za zamani za nyuklia
licha ya harakati za kimataifa za kupunguza silaha hizo husuan mkataba
wa NPT unaosisitiza kupunguzwa na hatimaye kuangamizwa kabisa silaha
hizo. Katika uwanja huo Washington imetenga bajeti ya dola bilioni 355
ambazo zitatumika kusasisha na kuboresha mitambo yake ya silaha na
kuinua juu kiwango cha majaribio ya silaha za nyuklia. Vilevile Marekani
imechukua hatua za kuboresha silaha na maghala yake ya zana za nyuklia
barani Ulaya yakiwemo mabomu ya nyuklia ya B-61.
Kwa
utaratibu huo, Washington, kinyume na mikataba ya kimataifa ya kuzuia
uzalishaji wa silaha za nyuklia, inaendelea kuzalisha na kufanyia
majaribio silaha za aina hiyo, suala ambalo linakiuka mkataba wa NPT.
CHANZO: IRAN SWAHILI
No comments:
Post a Comment