Siku
moja baada Katibu wa itikadi na Uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM)
Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza
kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa
yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo Mhe
Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji
imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.
Mhe
Lowassa anatoa kauli hiyo katika muendelezo wa kupokea makundi
mbalimbali ya jamii kumshawishi kuwania nafasi urais ambapo safari hii
waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 60 na wananchi wa
kawaida wamefunga safari kutoka wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya mpaka
mjini Dodoma kumshawishi agombee ambapo amesema kauli ya Nape Nnauye
inamshangaza kwani chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kujadili
mambo kama hayo kupitia vikao mbalimbali.
Mhe
Lowassa pia akawataka wanaoendelea kumnyooshea vidole kuhusu hatua ya
wananchi wenye imani naye kujitokeza kumshawishi awanie nafasi hiyo
wasubiri ufike wakati muafaka ili wana-CCM na wananchi waweze kutoa
maamuzi yao huku akisisitiza watu hasa vijana kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki
yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemuhitaji.
Awali
kundi hilo la vijana na bodaboda waliosafiri umbali wa kilometa zaidi ya
600 wakiongozwa na kamanda wa UV-CCM wilaya Mbarali Ibrahim Ismail
wamesema lengo la safari yao hiyo ni kuungana na watanzania wengine
kumtia moyo Mhe Lowassa ashawishike kuwania urais kwani wana imani kubwa
naye huku wakidai pamoja na mambo mengine kama alivyoweza kujenga shule
za kata nchi nzima pia ataweza kutegua bomu la tatizo la ajira hasa kwa
vijana.
-via ITV
No comments:
Post a Comment