Baadhi ya mabaki ya ndege ya Ujerumani aina ya Airbus A320 baada ya ajali.
ZOEZI
la utafutaji miili ya watu 150 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege
ya Ujerumani aina ya Airbus A320 yenye namba za usafiri 4U 9525
iliyoanguka jana katika Milima ya Alps, Ufaransa limeendelea leo huku
kifaa cha kunasia sauti kikipatikana huku kikiwa kimeharibika.
Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo la tukio.
Waziri
wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa
kifaa hicho cha kunasa sauti kwenye ndege kilipatikana jana Jumanne
baada ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Ujerumani ikitokea
Hispania.
Mbali
na kuharibika, Waziri Cazeneuve amesema kuwa kifaa hicho bado kitatoa
taarifa kwa wataalam wanaojaribu kubaini kilichosababisha kuanguka kwa
ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege
hiyo.
Helikopta zimeonekana zikipaa katika eneo la tukio huku maofisa wa polisi wakiendelea kuchunguza mabaki ya ndege hiyo.
Maofisa
wakuu wanaonya kuwa kupata mabaki ya miili ya abiria itachukua muda
mrefu kutokana na hali mbaya ya anga katika eneo hilo.
Kansela wa Ujerumani pamoja na Rais wa Hispania na waziri wake mkuu, wanatarajiwa kuzuru eneo la ajali hiyo leo Jumatano.
No comments:
Post a Comment