Mwenyekiti
wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com
Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi.
Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa
NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi
ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia
jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari
Maelezo Dar es Salaam.
On Friday, February 27, 2015
No comments
RAIS
KIKWETE
NA
MAKAMU
WAKE
WAAGA
MWILI
WA
MAMA
WA
DK
HOSEA
JIJINI
DAR
WANANCHI
WA
MKOA
WA
NJOMBE
NI
MFANO
WA
KUIGWA
KATIKA
ZOEZI
LA
Kazi
ya kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kupitia
mfumo wa Biometrick Voters Registration (BVR), ambao huhusisha uchukuaji
wa alama za vidole na picha, jana iliingia siku ya tatu, huku baadhi
yao wakipongeza utendaji wake.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyokusanywa na mwandishi wetu inasema kuwa tokea
siku ya kwanza lilipoanza zoezi hilo lilionyesha matumaini maana
wananchi wetu walijitokeza kwa wingi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi katika vituo vya uandikishaji, wananchi
hao walisema kuna mabadiliko ukilinganisha na siku zilizopita, hivi sasa
kazi zinafanywa haraka.
“Watu
wanaokwenda kwenye vituo kujiandikisha idadi yao ni kubwa kuliko hata
makadirio ya tume, kama hawataongeza muda au vifaa, siku saba
walizopanga, hazitatosha na wengi wataachwa bila ya kujiandikisha,”
alisema.
Baadhi
ya waandikishaji na wasimamizi wa mashine wameiomba Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) kuongeza muda ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi zaidi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la
Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati
ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu na Katibu
Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa
Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan
Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji
wa Daftarila Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada
ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika
mji mdogo wa Makambako.
Baadhi
ya watalaamu wa kuandikisha wapiga wakiwa na zana za kazi kabla ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uborereshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako.
On Friday, February 27, 2015
No comments
NIC
WAKABIDHI
ZAWADI
ZA
WASHINDI
MASHINDANO
YA
LUGALO
CHALLENGE
CUP
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu
katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC
Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia
saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji
mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mpaka
sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na
wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo
hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali
kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120
watashiriki katika mashindano hayo.
Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa
na shirika la bima la taifa NIC na linafanyika kila mwaka kuanzia
tangu lilipoanzishwa mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika
zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo
mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. Pia wshindi wengine
watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza
kubwa ya ofisini, mikoba ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni ,
Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akikabidhi zawadi kwa ya jiko kubwa la umeme Japhet Masai
Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta na Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya
gofu vya TPDF Lugalo wakipiga picha pamoja na zawadi hizo.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akipiga picha mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwenye
viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo.
On Friday, February 27, 2015
No comments
SOMA
JARIDA
LA
WIKI
LA
NISHATI
NA
MADINI,
TOLEO
LA
MKAZI
WA
DODOMA
JELA
MAISHA
KWA
KUNAJISNI
Tarehe 24/02/2015
katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, mtu mmoja anayefahamika
kwa jina la YUSUPH CHATAMBALA, umri miaka 45, kabila Mchaga, Mkulima na mkazi
wa Kijiji cha MAKUTUPA Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma,
amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la KUNAJISI mtoto wa miaka mine (4).
Mwendesha Mashitaka
wa Polisi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi GODWILL S. IKEMA (A/Insp) akisoma mashitaka
Mahakamani alisema, Mtuhumiwa alitenda kosa la KUBAKA lililo kinyume cha sheria
za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama
kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
YUSUPH CHATAMBALA alitenda kosa hilo siku ya
tarehe 20/02/2015 saa 12:00 jioni, huko kijiji cha Makutupa Wilaya ya Mpwapwa
Mkoa wa Dodoma, ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye miaka 04 (jina
limehifadhiwa). Alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na
watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi
kisha KUMNAJISI mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.
Mtuhumiwa
alifikishwa mahakamani siku ya tarehe 23/02/2015 na kusomewa shitaka lake,
ambapo alikiri kutenda kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
ya Wilaya ya Mpwapwa Mh. PASCHAL F. MAYUMBA. Siku ya tarehe 24/02/2015
alifikishwa tena Mahakamani hapo na kusomewa tena shitaka lake na kukiri tena
kutenda kosa hilo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mh.
PASCHAL F. MAYUMBA alimtia hatiani
mtuhumiwa huyo baada ya kukiri kutenda kosa hilo. Akisoma hukumu hiyo; Mh.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, alisema Mahakama inamhukumu
kwenda Jela Kifungo cha Maisha kwa
kosa la Kumnajisi mtoto ili kuwa
fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi D. A. MISIME – SACP alithibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na hukumu iliyotolewa dhidi ya mtuhumiwa huyo. Kamanda
Misime alisema Makosa ya Unyanyasaji wa Kijinsia yamekuwa yakichukuliwa hatua
kali kutokana na uelewa wa wananchi juu ya ubaya wa vitendo vinavyofanywa na
kutolea taarifa bila woga katika Madawati yanayoshughulikia kesi hizo katika
vituo vya Polisi. Alisisitiza kuwa wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la
Polisi kuwafichue wahalifu wa makosa yote na kuyafanya makazi yao kuwa sehemu
salama ya kuishi na kujiletea maendeleo bila hofu dhidi ya wahalifu.
Imetolewa na Idara ya Habari na Matukio Polisi Mkoa wa
Dodoma.
KNY: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Picha iliyotumika ni ya Gereza Kuu la Kigali Nchini Rwanda
Picha iliyotumika ni ya Gereza Kuu la Kigali Nchini Rwanda
On Thursday, February 26, 2015
No comments
PATO
LA
TAIFA
LAONGEZEKA,
LAFIKIA
SHILINGI
TRILIONI
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke (Kulia)akitoa taarifa ya Pato la
Taifa kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 leo jiji Dar es salaam. Pato hilo
kwa mwaka 2014 limefikia kiasi shilingi trilioni 21.2 kutoka trilioni 19.8 za mwaka 2013, Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Gregory Milinga,
Pato la Taifa
(GDP) katika kipindi cha robo ya tatu ya
mwaka 2014 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 21.2 kutoka shilingi trilioni 19.8 za kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jiji Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke, amesema kuwa katika kipindi
cha robo tatu ya mwaka 2014 sekta nyingi za uchumi zimefanya vizuri katika
uzalishaji ikilinganishwa na mwaka 2013.
Amesema katika kipindi
hicho shughuli za uchimbaji wa Madini , Mawe na Kokoto zimekua kwa asilimia 5.2
ikilinganishwa na asilimia 3.3 za mwaka 2013, Uzalishaji wa bidhaa za viwandani
ukikua kwa asilimia 10.8 kutoka asilimia
10.4 pamoja na ongezeko la uzalishaji wa umeme kwa asilimia 10.7 kutoka asilimia
10.3 za mwaka 2013 kutokana na matumizi ya mafuta na Gesi.
Amezitaja sekta
nyingine kuwa ni usambazaji maji ambao umekua kwa asilimia 12.7 kutoka 6.9 za
mwaka 2013, Habari na Mawasiliano kwa asilimia 11.9 kutoka 7.0, Shughuli za
Fedha na Bima zikikua hadi kufikia asilimia 13.9 kutoka asilimia 6.8 za mwaka
2013.
Ameongeza kuwa katika kipindi hicho huduma za upangishaji wa nyumba
zilikua hadi kufikia asilimia 2.2 kutoka 2.1, shughuli za kitaalamu, kisayansi, ufundi na
utawala zikifikia asilimia 5.4 kutoka asilimia 1.0 ya mwaka
2013.
Bw. Oyuke amezitaja shughuli
nyingine kuwa ni uendeshaji wa Serikali ambazo zilikua kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na 4.4,
huduma za Elimu kwa asilimia 3.7 kutoka 3.5, Afya kwa asilimia 8.1 pamoja na
shughuli za Sanaa na Michezo ambazo zilikua kwa asilimia 2.5 ikilinganishwa na 1.6
ya mwaka 2013.
Aidha, amebainisha
kuwa uzalishaji wa Almasi katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 ulikuwa
karatasi 66,508 ikilinganishwa na karatsi 27,828 zilizozalishwa katika kipindi
kama hicho mwaka 2013.
Akizungumza kuhusu
sekta ambazo hazikufanya vizuri katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2014 Mkurugenzi
huyo amesema kuwa ni dhahabu ambayo uzalishaji wake ulifikia Kilogramu 10,137
kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na 11,010 za mwaka 2013,Madini ya Tanzanite
kilogramu 1,449 kutoka 5140 zilizozalishwa mwaka 2013.
Amefafanua kuwa
shughuli za Biashara za Jumla na reja reja, Ukarabati wa magari na pikipiki
pamoja na vifaa vingine vya nyumbani zimeonyesha kukua kwa asilimia 6.0 kwa mwaka
2014 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 6.7 ya mwaka 2013, shughuli za uhifadhi
asilimia 13.9 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 19.3 za mwaka 2013.
Aidha, amebainisha
kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya mwaka 2014 kuanzia Julai mpaka
Septemba, Pato la taifa kwa bei za mwaka 2007 limefikia kiasi cha Shilingi trilioni
10. 7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 10.1 ya mwaka 2013.
On Thursday, February 26, 2015
No comments
MANISPAA
YA
TEMEKE
YA
MWAGA
KINYESI
ALICHO
HIFADHI
MWALIMU
WA
KIBASILA
CHUMBANI
Ama
kweli ukistaajabu ya musa hakika utayaona ya firauni...na kuishi kwingi
ni kuona mengi...hali kadhalika wahenga wanasema Tembea uyaone...Misemo
hiyo mitatu inaweza kujidhihirisha kwa namna tofauti tofauti kupitia
tukio la mkazi wa Jiji la Dar es salaam ambaye ni Mwalimu wa kike katika
shule ya Sekondari Kibasila iliyopo hatua kadhaa kutoka Manispaa ya
Temeke kubainika ndani kwake alipokua akiishi huko Yombo,
Kisiwani Kata ya Sandari kuwa kuna shehena ya kinyesi cha binadamu
katika ndoo, mabeseni, chupa za soda, maji pamoja na majagi.
Pichani
juu ni Wafanyakazi wa usafi wa Manispaa ya Temeke wakibeba kinyesi
kwenda kukimwaga baada ya kuvunja nyumba aliyokuwa akiishi Mwalimu
Gaudencia Albert.
Ubebabi kinyesi ukiendelea
Shehena ya kinyesi iliyokuwa chumbani kwa mwalimu huyo.
********
Manispaa ya Temeke jana Februari 25, 2015, imeteketeza kinyesi kilichokutwa
katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert
baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya
za wakazi wa eneo hilo.
Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo
la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la
Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi
hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo
walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa
Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani. SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HABARI MSETO BLOG
On Thursday, February 26, 2015
No comments
CHID
BENZ
ALIPA
FAINI
900,000/=,
AACHIWA
HURU
NA
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid
Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na
madawa ya kulevya.
Chid
Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo
misokoto ya bangi.
Mwanamuziki
huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo
akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la
muziki.
CHIDI
BENZ HURU:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki
'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya
kulevya. SOURCE: GPL
On Thursday, February 26, 2015
No comments
Tamthilia
ya
"A
Boys
Mission"
yahitaji
Milioni
800
ili
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye
vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa
tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana katikati
akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo
vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kushoto ni
Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na
Victor Casmir.
Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.
*****
Kampuni
mpya katika utengenezaji wa filamu nchini, Forward Formidable Enterprises (FFE)
inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” inahitaji kiasi cha
Sh milioni 800 ili ikamilike.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya FFE, Johnson Lujwangana alisema kuwa kwa sasa wameweza
kutengeneza toleo la utangulizi "pilot episode' kwa ajili ya kuonyesha
nini wanakifanya huku kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya kurekodiwa. Johnson
alisema kuwa tamthilia yao inazungumzia changamoto na suluhisho mbalimbali kwa
maisha ya vijana nchini na fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kughalimia
gharama mbalimbali za kuzalisha rasmi tamthilia hiyo.
Baadhi
ya gharama hizo kwa mujibu wa Johnson ni kulipa mtayarishaji bora, kuwalipa
wasanii fedha kutokana na ubora wa kazi zao, kulipia vifaa vya kisasa, kulipa
sehemu bora ya kurekodi tamthilia, usafiri, chakula na gharama nyinginezo.
“Kama
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond anatengeneza video ya dakika tatu kwa
Sh Milioni 60, kwa nini tamthilia ambayo kila sehemu (episode) inatumia si
chini ya dakika 45 hisifikia kiwango hicho cha fedha? Alihoji Johnson. Alisema
kuwa wao wanataka kuwafaidisha wasanii wao kwa kuwalipa vizuri na kuendelea
kudumu katika fani na kuwataka wadhamini kujitokeza kwa wingi kusaidia mradi
huo.
“Hakuna
hata msanii mmoja maarufu katika tamthilia hii, lengo si kama kuwatupa wasanii
hao, bali ni kupanua wigo na kuwapa nafasi wasanii wengine, nataka kizazi kipya
zaidi katika tasnia ili kuendeleza kuzalisha mastaa,” alisema. Alisema
kuwa katika tamthilia imeonyesha na kutoa majibu ya nini vijana wanatakiwa
kufanya hapa nchini na kuachana na fikra za kukimbilia nje ya nchi kwa kudhani kuwa ndiko kutakuwa suluhisho la
matatizo yao.
Alifafanua
kuwa mara baada ya kufika huko, hali inakuwa tofauti na kukutana na changamoto
nyingi zaidi za maisha na kuwaza kurejea nchini. “Tamthilia
ni ya kisasa zaidi kwani lengo letu pia ni kuonyeshwa nje ya nchi na kuonyesha
madhari ya kuvutia ya jiji letu la Dar es Salaam na kupromoti mji wetu tofauti
na hali iliyozoeleka kwani tamthilia nyingi uonyesha maisha ya vijijini,”
alisema Johnson.
Alifafanua
kuwa kwa kuonyesha usafi wa mji, maeneo mbalimbali ya starehe ya hapa nchini,
kutawavutia hata wasanii watayarishaji wa tamthilia nje ya nchi kuja
kutayarishia kazi zao hapa nchini. Alisema
kuwa tamthilia hiyo ina jumla ya sehemu 12 ambapo katika kila sehemu, muigizaji
mkuu ma maudhui ya tamthilia pia yanabadilika.
On Thursday, February 26, 2015
No comments
ZIARA
YA
WAZIRI
MKUU
PINDA
MBEYA
MJINI
NA
MBEYA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka
jiwe la Msingi la zahanati ya Kimondo , Mbeya Vijijini akiwa katika
ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25, 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Mjini Dr. Norman Sigalla.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Kimondo, Mbeya Vijijini kabla ya
kuweka jiwe la Msingi la zahanati yao akiwa katika ziara ya mkoa wa
Mbeya Februari 25, 2015. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbeya Vijijini,
Luckson Mwanjale na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman
Sigalla.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akikagua soko Kuu la Mjini Mbeya la Mwanjelwa baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25,
2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akiwasikiliza wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwambe mjini Mbeya
wakati alipofungua na kukagua maabara tatu za shule hiyo akiwa katika
ziara ya mkoa wa Mbeaya Februari 25, 2015. Kushoto ni mkewe Tunu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na wananchi baada ya kufungua vyumba vitatu vya Maabara
katika shule ya sekondari ya Songwe mkoani Mbeya Febrari 25, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Max Oswald (kushoto) na Ivan Kina
wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda katika kijiji cha Igoma , Mbeya Vijijini Februari 25,
2015.
On Thursday, February 26, 2015
1 comment
SHULE
ZA
MSINGI
MKOANI
SINGIDA
KUPOKEA
VITABU
Miss
Singida na Miss Kanda ya Kati 2014/15 ,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka
kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali
wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.
*********
SHULE tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii
kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu
hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book
Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika
kuwakomboa kielimu.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book
Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa
kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya
kunufaika zaidi kielimu.
"Watoto
wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi
ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze
kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani
Msaada
huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku
serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu.
Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania
hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa
shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.
Tafiti
mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa
kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani
elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha
yake ya baadae.
Kwa
upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida
anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake
mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake
nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na
Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za
msingi.
"Msingi
wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na
umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya
mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris
Doris
Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika
kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya
kitamaduni.
On Wednesday, February 25, 2015
No comments
ATUHUMU
POLISI
KUMVUNJA
MKAZI wa
Loksale wilaya ya Monduli, Samwel Petro Shani(47) amelalamikia hatua ya kuvunjwa mikono yake miwili kwa kipigo cha askari
polisi katika kituo cha Leskale kwa madai ya kushindwa kulipa deni
ya shilingi 250,000 alizokuwa akidaiwa ana mfanyabiashara wa eneo
hilo.
Aidha anawatuhumi askari hao kukodiwa na mfanyabiashara mmoja mkazi wa eneo hilo kwa lengo la kumshikisha adabu baada ya mkazi huyo kushindwa
kulipa deni la sh,250,000 alizokuwa akidaiwa na mfanyabiashara huyo.
Samweli ameeleza kupokea kipigo hicho ambapo alidai kuwa dhamira ya askari hao ilikuwa ni kumtoa uhai wake kwani walikuwa wakitumia chuma kinene kumpiga na kumvunja mikono yake miwili huku mwingine alikuwa akimshambulia kwa runngu na mateke.
Akizungumza kwa majonzi na gazeti hili jijini hapa,alieleza kuteswa na askari hao wanaodaiwa kukodiwa na mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina moja la bi Shamimu,ambaye alikuwa akimdai kiasi hicho cha fedha.
Alieleza kuwa tukio hilo lilitokea februali 6,mwaka huu majira ya saa 3 usiku na kwamba aliwatambua askari wawili waliomtesa kwa kipigo kuwa ni Steven na Justini wote ni askari wa kituo hicho cha Loksale.
''Mnamo tarehe 6 mwezi huu majira ya saa 3 usiku,walikuja askari wawili wakiwa wamevaa nguo za kiraia ,walinikuta nimekaa kwenye ukuta nikiwa na kijana mmoja,walinikamata na kunifunga pingu wakiwa wamenikandamizia chini ,walinipiga sana na kunivunja mikono yangu miwili''alisema Samweli
Akisimulia chanzo cha tukio hilo alisema ,mfanyabishara bi Shamimu alienda katika kituo hicho cha polisi na kuwaeleza askari hao kuwa alikuwa akinidai shilingi 250,000 na kwamba sikuwa nimemlipa deni hilo.
''Ni kweli Shamimu alikuwa akinidai shilingi 250,000 ila nilisha mlipa shilingi laki moja na kubaki sh,150,000 ,hizo hela kuna msichana nilimdhamini alikuwa mfanyakazi wa duka lake aliyedai alimwibia ,ndipo mimi kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na msichana huyo nilikubali kulilipa deni hilo''alisema Samweli
Alisema askari hao walimvamia na kumkaba kabali kisha askari mmoja alimfunga pingu na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na rungu na chuma na walipoona wamepoteza fahamu baada ya kumvunja mikono walimkokota hadi kituo cha polisi na kuendelea kumpigasehemu zingine za mwili ikiwemo miguuni.
''baadae usiku wakiwa wamenifungia lokapu alikuja mkuu wa kituo na kuniangalia ,alikuta hali yangu ni mbaya na kuondoka bila kusema lolote''alisema.
Hata hivyo askari hao waliingiwa na woga kutokana na hali yake na kuamua kumchukua usiku huo wa manane na kumpeleka katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.
Alieleza kuwa kesho yake askari hao walimchukua na kumpeleka kituo cha polisi wilaya ya Monduli na kumwoka lokapu.Aliongeza kuwa mkuu wa upelelezi wa wilaya OC CID,aliyemtaja kwa jina moja la bw Abichi alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila alitakiwa akibaliane na masharti ya dhamana .
''oc cid aliniambia kuwa nataka nikupatie dhamana ila kwenye maelezo yako unatakiwa ueleze kuwa ulikuwa unatoroka ulinzi halali wa polisi ukiwa na pingu ,na wakati ukikimbia ulianguaka na pingu zikakuvunja mikono yako ''alisema bw Shani.
Aliongeza kuwa hakukubaliana na kauli hiyo ndipo oc cid alipoamua kumrudisha lokapu ,ambapo alikaa kwa muda wa siku nne wakimbembeleza akubaliane na maelezo ya polisi .
Alisema kuwa aliamua kuwa na msimamo huo ,hadi tarehe 12 walipoamua kumfikisha mahakama ya wilaya ambapo alisomewa shtaka ,la kuvunja na kuiba na kujaribu kutoroka polisi akiwa na pingu ,suala ambalo ni uongo uliolenga kupoteza haki yake ya kulalamikia jeshi hilo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa alipotafutwa alikiri kupata malalamiko ya mkazi huyo ,hata hivyo alieleza kuwa kwa sasa yupo likizo ila aliwasiliana na mkuu wa kituo cha polisi Monduli(OCD)ili kupata undani wa tukio hilo.
Kwa upande wa mfanyabiashara ,Shamimu alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi alikana kukodisha askari wa kumpiga na kumvunja mkono mlalamikaji ila alieleza kuwa yeye alienda kituoni hapo kupeleka malalamiko yake ,ndipo askari hao walipoamua kumfuata mtuhumiwa na kwamba kilichotokea huko yeye hafahamu.
habari picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog
On Wednesday, February 25, 2015
No comments
BAADA
YA
KUIPANDISHA
MWADUI
FC
JAMHURI
KIWELO
'JULIO'
ATIMKIA
COAST
Kocha
Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri Kiwelu "Julio"kulia akisisitiza jambo
mazoezini jana mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu
hiyo kushoto ni Kocha Mkuu James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na
Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kocha
Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri Kiwelu "Julio"akizungumza na
viongozi wa Coastal Union mara baada ya kuwasili mazoezini jana.
On Wednesday, February 25, 2015
No comments
No comments:
Post a Comment