Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya
ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015
katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita
za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa
ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia
katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.
Hata
hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake
inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa
maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika
mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na
matibabu ya kawaida .
Wananchi
wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama
kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya
binadamu, nyumba wala miundo mbinu.
Baadhi
ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa
eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.
No comments:
Post a Comment