Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni Ya Samsung Tanzania Mike Seo akibadilishana Mkataba
na Msanii Vanessa Mdee pamoja na Meneja wake Michele Baldini.
Vanessa
Mdee akiwa katika picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Samsung Tanzania Mike Seo, Silvester Manyara Meneja Mauzo na Usambazaji
wa Samsung Tanzania pamoja na Meneja wa Vanessa Mdee Michele Baldini
Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akimkabidhi simu msanii wa Muziki Tanzania Vanessa Mdee
Mike Seo Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Tanzania akitia Saini Mkataba wa makubaliano baina yao na Msanii Vanessa Mdee
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania akiongea na wanahabari
Vannessa Mdee akiongea na wanahabari
Dar es Salaam, 16 Januari 2015; Kampuni
ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo
na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja
duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo
furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa
Televisheni na radio Vanessa Mdee.
Katika
mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko
mjini Dar es Salaam iliohusisha kusaini kwa mkataba baina ya Vannesa
Mdee na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara tosha ya makubaliano
rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho
kilihashiria mwanzo wa kazi mpya kwa Vanessa Mdee kama mwakilishi wa
kampuni ya Samsung nchini Tanzania.
Akiwa
kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika
muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya
Samsung, Mheshimiwa Mike Seo alisema kuwa, "kwa kutambua ongezeko la
uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora
kuwasiliana na wateja wetu kupitia mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana
na vifaa vyetu na soko letu. Anaongeza kuwa "Tunafuraha sana kutangaza
ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini
Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi
wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni
mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi
tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "
Vanessa
Mdee ambaye aliongozana na menejimenti yake kwenye mkutano huo,
alielezea juu ya furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung,
alisema "Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima
kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza
vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015
utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung. Binafsi,
natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi
rasmi. "
Kuhusu ya Samsung .
Samsung
Electronics Co., Ltd. Ni kampuni gwiji la vifaa vya kieletroniki
linalofungua milango kwa watu duniani. Kupitia uvumbuzi na ugunduzi
tunabadilisha ulimwengu wa TV, simu za kisasa, tablets, kompyuta,
kamera, printa na vifaa vya nyumbani. Na tumetoa jira kwa zaidi ya watu
286,000 katika nchi mbali mbali duniani na makadirio ya mapato yapatayo
dola bilioni 216.7. Tembele tovuti yetu kupata maelezo zaid kuhusu
kampeni yetu. www.samsung.com.
Kuhusu Vanessa.
Juu
ya mwendo wa kazi zake, muimbaji wa Tanzania, mtunzi wa nyimbo, na
mwanamuziki nyota Vanessa ametoa nyimbo tano ikiwa ni pamoja na Closer,
Hawajui, Come Over, Wave Clap dance na Siri, pia ameshirikishwa katika
nyimbo kama Me and you na Ommy Dimples, Money na AY, Monifere na Gosy B,
Bashasha na Bob Junior na Nisamehe na Angle. Vanessa alishinda tuzo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na tuzo nne za Kill Music Awards na moja ya
Afrika all Music Award. Amekuwa akijihusisha na kampeni mbalimbali kama
vile Staying Alive Foundation Project, kampeni ya Zinduka, MTV Africa
Music Awards, Sauti Za Busara, UNAIDS Mkutano wa vijana Mali uliofanyika
Bamako, Mkutano wa Kimataifa juu ya VVU na magonjwa ya zinaa ulofanyika
Addis Ababa, Ethiopia. Mdee amekuwa akiendesha vipindi kama MTV Base
meets, shoo inayolenga kuwawezesha vijana Waafrika kutoka duniani kote
kwa kuwapa fursa ya kukaa chini na kiongozi mashuhuri, Kili Music
Awards, Epiq Bongo Star Search (EBSS), Dume Challenge, 'Switch On'
kampeni ya Airtel, Coke Studio Afrika, Kili Music Tour, Serengeti Fiesta
Music Tour, Coca Cola Chart Express, The Hit ya Choice FM, pan-African
TV show na MTV Base select 10. Alishawahi kupata tuzo katika Gala mjini
New York kutoka kwa UNA-YP, alituzwa na GAVI Alliance kwa msaada wake
katika uanzishwaji wa chanjo bure kwa watoto wa Tanzania. Mdee balozi wa
GAVI na mpambanaji dhidi ya kansa ya kizazi. Mwaka 2014 alipata mkataba
kutoka kampuni ya Crown Paints, kuwa balozi wake nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment