Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu.
Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo
Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
====== ====== ===== =======
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa
ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s
Liberation Movement (SPLM), mgogoro ambao ulisababisha kuzuka kwa vita
ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata
hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na
Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika
mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania
hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo
yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais
Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa
Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada
za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani
ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza
mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo imegawanyika na
kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais
Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati
alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye
Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na
Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini
Tabora.
“Ni
fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na
Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu. Ni jambo la faraja
kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi
jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya
kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu
zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo.
Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro
tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”
No comments:
Links to this post