Waziri
Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akiwahutubia washiriki mbalimbali
kutoka barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Kumi wa
Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa
Speke Munyonyo Kampala, Uganda.
Washiriki
kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika
Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika
Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. Kushoto ni Mkuu wa
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda, katikati
ni Meneja wa Takwimu za Kilimo Titus Mwisomba kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Prof. Milline Mbonile.
Washiriki
wengine kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea
katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyonyo Kampala, Uganda. Kushoto ni
Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya akifuatiwa na Dkt.
Camilius Kasalla kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
Waziri
Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akimpongeza Mwandishi wa Kitabu
cha Mapinduzi ya Takwimu Afrika Prof. Ben Kiregyera baada ya kukizindua
leo kwenye Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika
katika ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. (PICHA NA
VERONICA KAZIMOTO - KAMPALA)
No comments:
Post a Comment